title : WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA BIASHARA LA KOREA NA TANZANIA
kiungo : WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA BIASHARA LA KOREA NA TANZANIA
WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA BIASHARA LA KOREA NA TANZANIA
*Aalika wawekezaji kwenye viwanda vya kuongeza thamani ya mazao
*Ataka waangalie fursa za uwekezaji zilizopo kwenye sekta ya utalii
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaalika wafanyabiashara kutoka Korea Kusini waanzishe miradi ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda kwa kushirikiana na wawekezaji wa ndani.
Ametoa mwaliko huo leo (Jumatatu, Julai 23, 2018) akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon wakati akifungua Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Korea lililofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kongamano la kwanza lilifanyika jijini Seoul, Februari 2018.
Amesema Serikali inahamasisha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vinavyotumia rasilimali za ndani ambavyo vitasaidia kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo, misitu, madini na bahari.
“Tunakaribisha uwekezaji wa viwanda katika maeneo ya uanzishaji wa viwanda vya kuzalisha bidhaa za walaji (consumer goods), pamoja na viwanda vya kuunganisha bidhaa mbalimbali, yaani (assembling plants) kama vile magari, simu na majokofu,” amesema.
Waziri Mkuu pia aliwaalika wafanyabiashara kutoka Korea waliohudhuria kongamano hilo waje kuwekeza kwenye sekta ya utalii ambako alisema kuna vivutio vya mbuga za wanyama kama Serengeti, Mlima Kilimanjaro, Olduvai Gorge na fukwe za bahari za Tanzania bara na Zanzibar.
“Tanzania ina kilometa 1,200 za fukwe kuanzia Tanga hadi Mtwara, ziko pia fukwe za Zanzibar, ziko fukwe kwenye maziwa yetu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa ambazo ni kivutio kingine cha utalii,” amesema.
Amesema ili kusimamia matumizi ya fukwe hizo, Serikali inakamilisha uundaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Fukwe kama ilivyo ile ya Ngorongoro ambayo alisema taratibu zikikamilika, itaanza kazi hivi karibuni.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji Kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Julai 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak- yon akihutubia katika Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji Kati ya Tanzania na Korea kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Julai 23, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mgeni wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak - yon (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji Kati ya Tanzania na Korea kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Julai 23, 2018. Kushoto kwa Waziri Mkuu Majaliwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA BIASHARA LA KOREA NA TANZANIA
yaani makala yote WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA BIASHARA LA KOREA NA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA BIASHARA LA KOREA NA TANZANIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-mkuu-afungua-kongamano-la-pili.html
0 Response to "WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA BIASHARA LA KOREA NA TANZANIA"
Post a Comment