title : PASS NA TALIRI WAJIPANGA KUONGEZA BIDHAA YA NYAMA KATIKA JIJI LA DODOMA
kiungo : PASS NA TALIRI WAJIPANGA KUONGEZA BIDHAA YA NYAMA KATIKA JIJI LA DODOMA
PASS NA TALIRI WAJIPANGA KUONGEZA BIDHAA YA NYAMA KATIKA JIJI LA DODOMA
Na Dixon Busagaga ,Dodoma.
TAASISI ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) imetumia fursa ya mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kuingia mashirikiano na Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ( PASS) ya kuwekeza katika sekta ya Mifugo kwa kuwaandaa Wajasiliamali vijana.
Hatua hiyo inatajwa kuondoa moja ya changamoto ya upatikanaji wa bidhaa ya Nyama katika jiji la Dodoma ambalo kwa sasa idadi ya watu imeanza kuongezeka baada ya ofisi na taasisi mbaimbali za serikali na umma kuhamia Dodoma.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini makubalinao hayo iliyofanyika katika kituo cha Kongwa Dodoma ,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo Nchini(PASS) ,Nicomed Bohay alisema PASS kupitia kituo cha ubnifu wa Biasharaza Kilimo wameamua kuanzisha Vituo atamizi vya Mifugo katika kituo cha TALIRI Kongwa .
“Tumelenga kuanza na mifugo aina ya Mbuzi katika kituo hiki ,zipo sababu zilizotupelekea tuweze kuchagua eneo hili la Kongwa moja wapo ni uwep wa soko la karibu ,… PASS tutawekeza kwenye Miundo mbinu ya ufugaji wa Mbuzi ,pamoja na gharama za kuendesha mradi na malisho hadi mbuzi watakapo weza kuuzwa sokoni .”alisema Bohay .
Alisema kazi hiyo itafanyika kwa kutumia wajasiliamali Vijana wa Kitanzania na kwamba utaratibu wa kuwapata vijana wenye sifa utatangazwa baadae na watakao pata nafasi hiyo watapata nafasi ya kuunganishwa na taasisi za kifedha kwa ajili ya kupata mitaji.
Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Kongwa Dodoma,Wilfredy Munisi akizungumza wakati wa utamburisho wa wagei waliofika katika kituo hicho kwa ajili ya hafla fupi ya utiaji saini katika makubaliano kati ya TALIRI na Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ( PASS) ya kusaidia Wajasiliamali Vijana katika sekta ya Mifugo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay (katikati) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini kati ya Taasisi hiyo na TALIRI ya kusaidia Wajasiliamali vijana.Kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Ubunifu katika Kilimo Biashara ,Tamim Amijee na kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima wasaini Makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo .Kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Ubunifu katika Kilimo Biashara ,Tamim Amijee na kushoto ni Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo Kongwa,Wilfredy Munisi.
Hivyo makala PASS NA TALIRI WAJIPANGA KUONGEZA BIDHAA YA NYAMA KATIKA JIJI LA DODOMA
yaani makala yote PASS NA TALIRI WAJIPANGA KUONGEZA BIDHAA YA NYAMA KATIKA JIJI LA DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PASS NA TALIRI WAJIPANGA KUONGEZA BIDHAA YA NYAMA KATIKA JIJI LA DODOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/pass-na-taliri-wajipanga-kuongeza.html
0 Response to "PASS NA TALIRI WAJIPANGA KUONGEZA BIDHAA YA NYAMA KATIKA JIJI LA DODOMA"
Post a Comment