WAZIRI LUGOLA AMPA MIEZI MINNE LUGUMI

WAZIRI LUGOLA AMPA MIEZI MINNE LUGUMI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI LUGOLA AMPA MIEZI MINNE LUGUMI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI LUGOLA AMPA MIEZI MINNE LUGUMI
kiungo : WAZIRI LUGOLA AMPA MIEZI MINNE LUGUMI

soma pia


WAZIRI LUGOLA AMPA MIEZI MINNE LUGUMI

*Ni wa kufunga mashine Polisi, akishindwa Mahakama ya Mafisadi inamsubiri*

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ametoa muda wa miezi minne kwa mmiliki wa Kampuni ya Lugumi ,Said Lugumi kuhakikisha anafunga mashine za utambuzi wa alama za vidole iwapo atashindwa ndani ya muda huo atampeleka Mahakama ya Mafisadi.

Lugola ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waaandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo na Lugumi ambaye alijisalimisha ofisini kwake baada ya kuagiza aripoti Julai 31 mwaka huu.

Lugola ameeleza kuwa Lugumi aliwasili wizarani hapo kama walivyopanga na kuzungumza kuhusu mkataba aliongia na Serikali wa ufungaji wa mashine hizo na katika mazungumzo hayo amempa muda huo na amekubali.“Lugumi tumekubaliana ndani ya miezi 4 atakuwa amekamilisha kufunga mashine hizo na akishindwa katika kipindi hiki hicho ajue Mahakama ya Mafisadi inamsubiri.

“Mnafahamu Rais ameanzisha mahakama kwa ajili ya mafisadi na tangu kuanzishwa kwake bado ina uhaba wa wateja.Hivyo Lugumi akishindwa ajue atakuwa mteja wa Mahakama hiyo ambayo bado inahitaji watu,”amesema Lugola.Alipolizwa kwanini amezungumza na Lugumi na kisha kumruhusu aondoke badala ya kumuweka mahabusu,Lugola amejibu si kola jambo lazima mtu awekwe mahabusu.

Amesema kuwa katika mkataba huo Serikali ilishatoa fedha zake na hivyo kinachohitajika ni kufungwa kwa hizo mashine au fedha na Lugumi amekubali kufunga mashine na ndio maana amempa huo muda.

Kuhusu mkataba baina ya Lugumi na Serikali Lugola amesema kwanza mkataba huo unashughulikiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) na Wizara ya mambo ya ndani wanamshughulikia Lugumi kwa kutapeli jeshi la polisi kwa kutomaliza kazi aliyopewa ikiwa amelipwa.


Hivyo makala WAZIRI LUGOLA AMPA MIEZI MINNE LUGUMI

yaani makala yote WAZIRI LUGOLA AMPA MIEZI MINNE LUGUMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUGOLA AMPA MIEZI MINNE LUGUMI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-lugola-ampa-miezi-minne-lugumi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI LUGOLA AMPA MIEZI MINNE LUGUMI"

Post a Comment