WAAJILI WATAKIWA KUTENGA CHUMBA MAALUM CHA KUNYONYESHEA.

WAAJILI WATAKIWA KUTENGA CHUMBA MAALUM CHA KUNYONYESHEA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAAJILI WATAKIWA KUTENGA CHUMBA MAALUM CHA KUNYONYESHEA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAAJILI WATAKIWA KUTENGA CHUMBA MAALUM CHA KUNYONYESHEA.
kiungo : WAAJILI WATAKIWA KUTENGA CHUMBA MAALUM CHA KUNYONYESHEA.

soma pia


WAAJILI WATAKIWA KUTENGA CHUMBA MAALUM CHA KUNYONYESHEA.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imewaagiza waajili wote wa Serikali na Sekta binafsi kutenga chumba maalum kwa ajili ya waajiliwa wao wanaonyonyesha.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akitoa Tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.“Ninazitaka Halmashauri zote nchini kupitia maafisa kazi kuhakikisha wanawake waajiriwa waliojifungua wanapata haki yao ya likizo ya uzazi na muda wa kunyonyesha kwa ukamilifu” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amewataka Wanaume wanaopewa likizo za uzazi kuzitumia ipasavyo kwa kumsaidia mama kazi ili aweze kumnyonyesha mtoto mchanga aliyejifungua badala ya ktumia likizo hizyo kwenda kukaa baa.Waziri Ummy alisema kuwa vituo vyote vinavyotoa huduma ya afya vinatekeleza vidokezo kumi vya kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama na hivyo kuwa rafiki wa Mtoto.

“Wazazi tunatakiwa kufuata taratibu za kunyonyesha ikiwemo kuanza kumnyonyesha mtoto ndani ya saa moja ya kwanza ya mama kujifungua, kunyonyesha mtoto mara kwa mara kadiri anavyohitaji, kuendelea kunyonyesha maziwa ya mama pekee bila kumpatia mtoto kitu kingine chochote hata maji katika miezi sita ya mwanzo na kuendelea kunyonyesha hadi anapofikisha umri wa miaka miwili au zaidi” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa takwimu za utafiti wa hali ya kidemografia na afya uliofanyika mwaka 2015 zinaonesha kuwa asilimia 59 ya watoto wenye umri wa miezi 0 hadi miezi 6 wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee.
“kila Mwajiri anatakiwa kumruhusu mfanyakazi mwanamke aliyejifungua kumnyonyesha mtoto wakati wa saa za kazi kwa jumla ya mpaka masaa 2 kwa siku kwa kipindi kisichopungua miezi 6 tangu kumaliza likizo yake ya uzazi” alisisitiza Waziri Ummy.

Kila ifikapo tarehe 1 – 7 Agosti ya kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine ulimwenguni kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama na maadhimisho yam waka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA NI MSINGI WA MAISHA.”


Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani kuhusu umuhimu wa kunyonyesha watoto wachanga wakati akitoa Tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa pilia kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya afya mara baada ya tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta ya afya wakimsikiliza Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati akitoa Tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)


Hivyo makala WAAJILI WATAKIWA KUTENGA CHUMBA MAALUM CHA KUNYONYESHEA.

yaani makala yote WAAJILI WATAKIWA KUTENGA CHUMBA MAALUM CHA KUNYONYESHEA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAAJILI WATAKIWA KUTENGA CHUMBA MAALUM CHA KUNYONYESHEA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waajili-watakiwa-kutenga-chumba-maalum.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAAJILI WATAKIWA KUTENGA CHUMBA MAALUM CHA KUNYONYESHEA."

Post a Comment