title : WAZIRI KIGWANGALLA ATOA SIKU 90 KWA TAWIRI KUFANYA SENSA YA MAMBA ZIWA RUKWA NA TFS KUANDAA MPANGO WA KITAIFA WA UVUNAJI MISITU
kiungo : WAZIRI KIGWANGALLA ATOA SIKU 90 KWA TAWIRI KUFANYA SENSA YA MAMBA ZIWA RUKWA NA TFS KUANDAA MPANGO WA KITAIFA WA UVUNAJI MISITU
WAZIRI KIGWANGALLA ATOA SIKU 90 KWA TAWIRI KUFANYA SENSA YA MAMBA ZIWA RUKWA NA TFS KUANDAA MPANGO WA KITAIFA WA UVUNAJI MISITU
Na Hamza Temba, Songwe
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kufanya utafiti na sensa ya mamba katika ziwa Rukwa ili kubaini idadi yake na hatimaye kuishauri Serikali namna ya kudhibiti madhara yanayosababishwa na mamba hao kwa wananchi hususan wa jimbo la Songwe ikiwemo kuwavuna kama idadi yao itabainika kuwa kubwa kupita kiasi.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana katika kijiji cha Maleza, kata ya Mbangala, wilaya ya Songwe mkoani Songwe alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili ya kutatua mgogoro uliopo baina ya wananchi na Mamba wa ziwa Rukwa.
"Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori ambayo ipo chini ya wizara yangu, nawaagiza wafike hapa mara moja, ndani ya miezi mitatu wanipe majibu nini kifanyike kupunguza madhara yanayotokana na mamba kwenye ziwa Rukwa, wafanye sensa watuambie kuna Mamba wangapi lakini pia watushauri nini tufanye ili kudhibiti mamba hao wasiendelee kusababiaha athari kubwa kwenye maisha ya watu wanaoishi jirani, lakini pia wanaoutumia ziwa.
"Kwa sababu madhara yanaweza yakawa mengi, inawezekana mamba wameshakuwa wengi na samaki wamebaki wachache, kwahivyo hata mamba nao mwishowe wataanza kufa ama wataanza kutafuta chanzo kingine cha chakula pengine ndio maana wameanza kutafuta binadamu wanakwenda ziwani kwasababu wanakuwa na njaa, inabidi wasogee ufukweni wawinde chochote kinachosogea karibu na maji" alifafanua Dk. Kigwangalla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Maleza kata ya Mbangala wilaya ya Songwe mkoani Songwe alipofanya ziara ya kikazi katika kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mamba wa ziwa Rukwa ambao wamekuwa wakidhiru wananchi wa kijiji hicho na vijiji jirani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akitoa agizo la kutaifishwa kwa greda (pichani nyuma) lililokutwa ndani Hifadhi ya Msitu wa Patamela baada ya kutelekezwa na watu watu wasiojulikana waliokuwa wakichimba mchanga wa dhahabu (makinikia) kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi hiyo katika wilaya ya Songwe mkoani Songwe jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa uongozi wa wilaya ya Songwe kufuatia greda lililokutwa ndani Hifadhi ya Msitu wa Patamela ambalo limetelekezwa na watu wasiojulikana waliokuwa wakichimba mchanga wa dhahabu (makinikia) kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi hiyo katika wilaya ya Songwe mkoani Songwe jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akishirikiana na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Songwe kuzima moto uliokutwa ukiwaka ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo jana.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI KIGWANGALLA ATOA SIKU 90 KWA TAWIRI KUFANYA SENSA YA MAMBA ZIWA RUKWA NA TFS KUANDAA MPANGO WA KITAIFA WA UVUNAJI MISITU
yaani makala yote WAZIRI KIGWANGALLA ATOA SIKU 90 KWA TAWIRI KUFANYA SENSA YA MAMBA ZIWA RUKWA NA TFS KUANDAA MPANGO WA KITAIFA WA UVUNAJI MISITU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KIGWANGALLA ATOA SIKU 90 KWA TAWIRI KUFANYA SENSA YA MAMBA ZIWA RUKWA NA TFS KUANDAA MPANGO WA KITAIFA WA UVUNAJI MISITU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-kigwangalla-atoa-siku-90-kwa.html
0 Response to "WAZIRI KIGWANGALLA ATOA SIKU 90 KWA TAWIRI KUFANYA SENSA YA MAMBA ZIWA RUKWA NA TFS KUANDAA MPANGO WA KITAIFA WA UVUNAJI MISITU"
Post a Comment