title : WAZIRI KANGI LUGOLA AWASHUSHA VYEO MAKAMANDA WAWILI
kiungo : WAZIRI KANGI LUGOLA AWASHUSHA VYEO MAKAMANDA WAWILI
WAZIRI KANGI LUGOLA AWASHUSHA VYEO MAKAMANDA WAWILI
Na Said Mwishehe
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ametangaza kuwashusha vyeo Makanda wa wawili kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao yakiwamo ya kushindwa kudhibiti ajali.
Lugola ametangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam akiwa katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kwamba hatua hizo ni kuonesha hayupo tayari kuacha makamanda na wakuu wengine wa Idara wafanya kazi kimazoea.
Hivyo amemshusha cheo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya pamoja na Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Kagera na wote hao umetokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao hasa ya ajali.
Lugola amesema Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya Leopard Funguo ambaye ni Mrakibu wa Polisi amemchukulia hatua kwa kumshusha cheo chake mara moja kutoka urakibu abaki na nyota tatu.
Amesema sababu za kumshusha cheo hicho kunatokana na kushindwa kuchukua hatua za kudhibiti ajali za barabarani.Pia amesema juzi mkoani Kagera kulitokea ajali ya moto katika Chuo cha Ufundi Lake Zone
Mrakibu Mwandamizi George Mrutu ambaye ni Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto katika Mkoa huo alipewa taarifa na uongozi wa chuo hicho ya kutokea kwa ajali ya moto. Lugola amesema kwa mujibu wa picha alizonazo na vyombo vya habari Mrutu anakiri kwa kinywa chake kuwa a hakwenda katika tukio kwa sababu hana gari ya zima Moto.
Amefafanua wakati huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Mkoa wa Kagera pamoja maofisa wengine wakionekana wakishirikiana na wananchi kuzima moto huo bila ya kuwa na gari la zima moto.
"Kutokana na tukio hilo nimejiuliza imekuaje ambao hawajapewa dhamana ya kisheria ya kuzimaa moto wanakwenda pale kuzima moto na wenye dhamana ya kisheria wakashindwa kushiriki kuzima moto huo,"amesema Lugola. Amefafanua zipo kazi ambazo kikosi cha Zimamoto na Uokaoji kuna mambo wanaweza kufanya bila hata kuwa na gari ya zima moto ikiwemo ya kutoa maelekezo ya kuwaepusha wananchi ya kukaa mbali na eneo la tukio la ajali.
Kabla ya kutangaza kumshusha cheo Lugola amempongeza Mkuu wa Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji nchini kwa kumuondoa kamanda wa Kikosi hicho Mkoa wa Kagera. Hata hivyo amesema kumuondoa katika nafasi hiyo peke yake haotoshi, hivyo akatangaza naye ashushwe cheo kimoja abaki na nyota tatu.
Amesema alikuwa ameamua wafukuzwe kazi wote na bahati yao yeye amezaliwa Ijumaa hivyo ameamua washushwe cheo tu badala ya kuwatimua.Pia amesema anatuma salamu kwa wakuu wa Polisi kutambua zama hizi si za mwaka 47 na kwamba chini ya utawala wa Rais John Magufuli hawatakuwa tayari kuvumilia mambo yaende bila utaratibu.
Hivyo makala WAZIRI KANGI LUGOLA AWASHUSHA VYEO MAKAMANDA WAWILI
yaani makala yote WAZIRI KANGI LUGOLA AWASHUSHA VYEO MAKAMANDA WAWILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KANGI LUGOLA AWASHUSHA VYEO MAKAMANDA WAWILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-kangi-lugola-awashusha-vyeo.html
0 Response to "WAZIRI KANGI LUGOLA AWASHUSHA VYEO MAKAMANDA WAWILI"
Post a Comment