Wafanyabiashara wa Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa Comoro

Wafanyabiashara wa Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa Comoro - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wafanyabiashara wa Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa Comoro, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wafanyabiashara wa Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa Comoro
kiungo : Wafanyabiashara wa Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa Comoro

soma pia


Wafanyabiashara wa Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa Comoro

Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Silvester Mabumba amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa za kibiashara nchini Comoro kwani mazingira ya kibiashara nchini humo ni mazuri sana.

Mabumba amesema kwamba Visiwa vya Comoro hutegemea nchi ya Tanzania kuagiza mahitaji yake yote ya msingi kama chakula, saruji, mbogamboga na vifaa vya kiwandani, haswa fenicha. Amesema hata kijiografia, Visiwa vya Comoro ndio vilivyo karibu zaidi na hutegemea Tanzania pekee kufanya nao biashara. Amesema biashara kati nchini zote mbili kwasasa imekuwa hadi kufikia Tsh500 bilioni.

“napenda kuchukua fursa hii, niwasihi wafanyabiashara wa Tanzania, watumie nafasi hii ya kipekee kwani Visiwa vya Comoro hutegemea kuagiza mahitaji yao yote ya chakula na bidhaa nyingine kutoka Tanzania pekee,” amesema Mhe. Balozi Mabumba.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema kwa upande wao kama Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wamejipanga kushirikiana na wadau kutatua changamoto zote zinazojitokeza kwa wafanyabiashara hao. Mhandisi Kakoko amesema kwamba TPA, kama muwezeshaji amejipanga kutoa huduma bora na kwa ufanisi mkubwa ili kukuza biashara kati ya nchi hizo na kusaidia kuongeza pato kwa TPA na serikali zote mbili kwa ujumla.

“huduma zikiwa bora na za haraka bandarini, huleta nafuu kwa mlaji na kuongeza mapato ya serikali, hivyo sisi kama bandari ziara hii kwetu imekuwa ya mafanikio makubwa kwani nimepata mambo ya kwenda kufanyia kazi zaidi ya niliyoyatarajia,” amesema Mhandisi Kakoko.

Mhandisi Kakoko amesema kwamba kwa kushirikiana na wenzo wa Comoro wataanza kwa kuboresha masuala ya kiusalama ambapo amesema kwamba watahakikisha kila meli au boti inayochukua bidhaa Tanzania kwenda Comoro inatumia radio maalumu za mawasiliano majini. Mbali na hilo amesema kwamba atahakikisha makubaliano yaliyofikiwa kati cha Moroco Chamber of Commerce na Tanzania Chamber of Commerce ya Mtwara yanatekelezwa ili kuboresha shughuli za ufanyaji biashara.

Mkurugenzi mkuu huyo wa TPA, pia aliahidi kuwasiliana na wenzao wa Zanzibar kuona jinsi meli zao mbili zinavyoweza kusaidia kusafirisha mizigo kati ya nchi hizo kwani ni salama zaidi na vumulivu. Visiwa vya Ngazidja na Anjouani ambavyo ndio vikubwa nchini Comoro kutegemea Tanzania kuagiza mahitaji yake yote ya msingi haswa chakula kwa asilimia 70. Comoro huagiza zaidi mchele na viazi, mbogamboga, saruji na bidhaa nyinginezo za viwandani.


Hivyo makala Wafanyabiashara wa Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa Comoro

yaani makala yote Wafanyabiashara wa Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa Comoro Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wafanyabiashara wa Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa Comoro mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wafanyabiashara-wa-tanzania-watakiwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Wafanyabiashara wa Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa Comoro"

Post a Comment