title : utalii katika msitu wa Chome kilele cha mlima Shengena wilayani Same kutangazwa
kiungo : utalii katika msitu wa Chome kilele cha mlima Shengena wilayani Same kutangazwa
utalii katika msitu wa Chome kilele cha mlima Shengena wilayani Same kutangazwa
Ni utalii katika msitu wa Chome hususan kilele cha mlima Shengena ambapo Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imedhamiria kutangaza kivutio hiki ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Rosemary Sitaki aliongoza wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakiratibiwa na Wakala wa Misitu (TFS) kupanda mlima Shengena wenye urefu wa Mita 2462 toka usawa wa bahari, ambacho ni kilele cha pili kwa urefu kufuatia Mlima Kilimanjaro.
Mlima huo una vivutio vingi vya miti, ndege, vipepeo, nyani, mito na uoto wa asili ni raslimali kubwa.
Ni eneo unaloona Mlima kilimanjaro kwa juu zaidi kuliko eneo jingine lolote, na linafaa kwa utalii, mazoezi ya kupanda mlima Kilimanjaro, kurekodi Sinema, hifadhi ya mazingira, uwekezaji, utafiti, vyanzo vya maji, camp site ambapo
TFS wanafikiria kuweka "sky line"
" Ni lazima tujipange kufanya vitu tofauti ili kuwafanya watalii kuchagua Shengena" alisema DC Sitaki, huku akiwaalika wananchi na wageni kuja kujionea uumbaji wa ajabu wa Mungu uliopo Shengena.
Alitoa tahadhari kwa wenye nia ya kuchezea msitu huo, kwa kuwa ni moyo ya Wilaya ya Same kwani vyanzo vya maji zaidi ya 8 vinavyotegemewa na Wananchi vinaanzia msitu huo. Aliahidi kuutunza, kuulinda kuuthamini na kuwachukulia hatua wanaouchezea.
Timu hiyo ilitumia kati ya saa 2.30 - 2.40 kufika kileleni umbali wa Km. 5.54.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Rosemary Sitaki (kilemba cha buluu) na wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakipumzika baada ya kupanda mlima Shengena wenye urefu wa mita 2462 kutoka usawa wa bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Rosemary Sitaki (kilemba cha buluu) akiongoza wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakipumzika baada ya kupanda mlima Shengena wenye urefu wa mita 2462 kutoka usawa wa bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Rosemary Sitaki (kilemba cha buluu) na wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakiwa kwenye kilele cha mlima Shengena wenye urefu wa mita 2462 kutoka usawa wa bahari.
Mtaalamu akitoa maelezo juu ya kilele cha mlima Shengena
Hivyo makala utalii katika msitu wa Chome kilele cha mlima Shengena wilayani Same kutangazwa
yaani makala yote utalii katika msitu wa Chome kilele cha mlima Shengena wilayani Same kutangazwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala utalii katika msitu wa Chome kilele cha mlima Shengena wilayani Same kutangazwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/utalii-katika-msitu-wa-chome-kilele-cha.html
0 Response to "utalii katika msitu wa Chome kilele cha mlima Shengena wilayani Same kutangazwa"
Post a Comment