title : TUMEANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA VITENDO-RC MASENZA
kiungo : TUMEANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA VITENDO-RC MASENZA
TUMEANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA VITENDO-RC MASENZA
Na Francis Godwin Michuzi Blog, Iringa
MKUU wa mkoa (RC) wa Iringa Amina Masenza amesema kuwa mkoa wake umeanza utekelezaji wa agizo la waziri mkuu Kasimu Majaliwa la kutaka wanaume kupimwa virusi vya UKIMWI ili kupunguza kasi ya maambukizi ya VVU nchini.
Akizungumza leo katika ukumbi wa siasa ni kilimo mara baada ya kuwaongoza wadau wa maendeleo mkoani Iringa walioshiriki kikao cha mikakati ya utekelezaji wa agizo la waziri mkuu kupima VVU ,Masenza alisema kuwa zoezi la upimaji wa VVU kwa wanaume mkoani Iringa litasaidia kuwatambua wale ambao wameambukizwa na kuanzishiwa dawa za ARVs huku wale ambao hawajaathirika kujikinga na VVU.
Alisema kuwa michango ya wajumbe wa kikao hicho iliyotolewa ya kutaka wanaume kuhamasishwa kupima VVU kwa hiari majumbani kwao ni michango ambayo itasaidia kufikia malengo ya mapambano dhidi ya UKIMWI iwapo wanaume wote mkoani hapa wataonyesha ushirikiano katika zoezi hilo pindi litakapo anza .
Alisema kuwa taarifa za mganga mkuu wa mkoa wa Iringa zinaonyesha tatizo la UKIMWI bado kubwa ndani ya mkoa na kuwa pamoja na ukubwa wa tatizo ila bado kuna wadau wengi wa mapambano ya UKIMWI .
Kuwa kampeni ya kitaifa ya upimaji wa VVU na utoaji wa dawa za kupumbaza VVU iliyozinduliwa na Juni 19 mjini Dodoma na waziri mkuu imekwenda sanjari inajumuisha na usemi usemao Furaha yangu pima jitambue hivyo kampeni hiyo itanaza kwa wanaume na baadae makundi mengine katika jamii .
Kuwa makundi hayo ni pamoja na mabinti wa miaka kuanzia 15 hadi 21 ,wanawake wajawazito na wengine wote na kuwa njia pekee ya kufanikisha kampeni hiyo ni wananchi wote kujitokeza kupima VVU .
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiongoza kupima VVU katika kikao cha mikakatiya kuanzakampeni za kupima UKIMWI kwa wanaume
Viongozi wa mkoa wa Iringa wakiwemo wakuu wa wilaya ya Mufindi na kilolo wakionyesha karatasi baada ya kupima VVU
Washiriki wa kikao cha kuweka mikakati ya zoezi la upimaji UKIMWI wanaume wakiwa katika kikao hicho.
Hivyo makala TUMEANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA VITENDO-RC MASENZA
yaani makala yote TUMEANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA VITENDO-RC MASENZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUMEANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA VITENDO-RC MASENZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tumeanza-utekelezaji-wa-agizo-la-waziri.html
0 Response to "TUMEANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA VITENDO-RC MASENZA"
Post a Comment