Tigo na HMD Global wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu

Tigo na HMD Global wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tigo na HMD Global wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tigo na HMD Global wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu
kiungo : Tigo na HMD Global wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu

soma pia


Tigo na HMD Global wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu

Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania imeungana na HMD Global, wauzaji wa simu za Nokia kuwapa wateja fursa ya kumiliki kw abei nafuu, simu janja zenye uwezo wa 4G  na intaneti bure kwa miezi sita kutoka Tigo.

Katika msimu huu wa Sabasaba, Tigo na HMD Global wanakuletea simu za Nokia 3310 kwa bei ya TSH 99,000, na Nokia 1 kwa bei pungufu ya TSH 174,999 pekee.

“Simu inayotumia laini mbili ya Nokia 3310 pamoja na simu janja ya Nokia 1 zote zinakuja na ofa ya GB 2 za intaneti kwa miezi sita kutoka Tigo,’ Woinde Shisael, Meneja Mawasiliano wa Tigo alisema katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika Maonyesho ya Dar es Salaam ya Kimataifa ya Biashara  katika viwanja vya JK Nyerere jijini Dar es Salaam.

Shisael aliongeza kuwa,“Tigo wanaongoza mabadiliko ya maisha ya kidigitali. Tunalenga kuongeza matumizi ya simu janja nchini na kuhakikisha kuwa wateja wetu wote wanafurahia huduma bora zaidi ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana na wenye kasi ya juu zaidi wa Tigo.”

Akizungumzia ushirikiano huo, Gopher Ogembo, Meneja wa Biashara wa HMD Global, Ukanda wa Africa Mashariki alisema, “Simu zetu zinaweka viwango vipya vya ubora na raha ya matumizi. HMD Global inaamini kuwa kila mteja anahitaji kupata bidhaa yenye viwango vya juu vya  ubora na umbo la kuvutia.

Ogembo aliongeza kuwa “Pamoja na kutengeneza bidhaa za kuvutia zinazolenga kuongeza raha ya matumizi kwa wateja, kila kifaa kinachotumika kutengeneza simu za Nokia kimetazamwa kwa undani zaidi ili kuboresha faida kwa maisha ya kila sikui ya mteja. Tunafurahia kufungua ukurasa mpya wa Nokia kwa wateja wetu wote nchini Tanzania. Simu mpya za Nokia zimetengenezwa kwa ajili ya kizazi kipya cha wateja kwa kuzingatia historia ndefu ya ubora, umathubuti na urahisi wa matumizi.”

Simu zote zinapatikana katika banda la Tigo lilipo katika Maonyesho ya Dar es Salaam ya Kimataifa ya Biashara  pamoja na katika maduka yote ya Tigo nchi nzima.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) na Meneja wa Biashara wa kampuni ya HMD Global inayosambaza simu za Nokia, Gopher Ogemb (kulia) wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe za simu kutoka Tigo na Nokia katika msimu huu wa Sabasaba. Tigo na Nokia wanatoa simu za kisasa kwa bei nafuu zenye ofa ya bando ya intaneti bure kwa miezi sita.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Nokia 1 kwa mwandishi wa habari Vumilia Mwasha (kulia) aliyoshinda katika droo ndogo iliyofanyika wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe za simu kutoka Tigo na Nokia katika msimu huu wa Sabasaba. Katikati ni Meneja wa Biashara wa kampuni ya HMD Global inayosambaza simu hizo za Nokia, Gopher Ogembo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Nokia 1 kwa mpiga picha Anthony Siame (kulia) aliyoshinda katika droo ndogo iliyofanyika wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe za simu kutoka Tigo na Nokia katika msimu huu wa Sabasaba. Katikati ni Meneja wa Biashara wa kampuni ya HMD Global inayosambaza simu hizo za Nokia, Gopher Ogembo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Nokia 1 kwa mwandishi wa habari, Ellen Manyangu (kulia) aliyoshinda katika droo ndogo iliyofanyika wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe za simu kutoka Tigo na Nokia katika msimu huu wa Sabasaba. Katikati ni Meneja wa Biashara wa kampuni ya HMD Global inayosambaza simu hizo za Nokia, Gopher Ogembo.


Hivyo makala Tigo na HMD Global wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu

yaani makala yote Tigo na HMD Global wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tigo na HMD Global wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tigo-na-hmd-global-wanaungana-kuleta.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Tigo na HMD Global wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu"

Post a Comment