TFDA YAWEZESHA MKOA WA KATAVI KUWA NA VIWANDA VINGI VYA UZALISHAJI VYAKULA

TFDA YAWEZESHA MKOA WA KATAVI KUWA NA VIWANDA VINGI VYA UZALISHAJI VYAKULA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TFDA YAWEZESHA MKOA WA KATAVI KUWA NA VIWANDA VINGI VYA UZALISHAJI VYAKULA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TFDA YAWEZESHA MKOA WA KATAVI KUWA NA VIWANDA VINGI VYA UZALISHAJI VYAKULA
kiungo : TFDA YAWEZESHA MKOA WA KATAVI KUWA NA VIWANDA VINGI VYA UZALISHAJI VYAKULA

soma pia


TFDA YAWEZESHA MKOA WA KATAVI KUWA NA VIWANDA VINGI VYA UZALISHAJI VYAKULA

 Picha ya pamoja baina ya Wajasiriamali Wadogo wa Usindikaji wa Vyakula mkoani Katavi, Watumishi wa TFDA, na wawezeshaji kutoka Taasisi za Serikali katika Ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili, tarehe 2 – 3 Julai 2018 katika Ukumbi wa Mkutano wa Idara ya Maji katika Halmashauri ya Mpanda. Waliokaa kutoka kushoto ni Mgeni Rasmi, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Huruma I. Mwalutanile (wa tatu); Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka TFDA, Bw. Justin Makisi (wa nne); Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Omari Sukari (wa pili); Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mali wa Mkoa wa Katavi, Inj. Awariywa Nko (wa tano); Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya Mpanda, Bi. Enelia Lutungulu (wa sita) na Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Katavi, Bi. Salome Mwasomola (wa kwanza). Waliosimama mbele, msitari wa pili kushoto ni Meneja wa TFDA Kanda ya Magharibi, Dkt. Edgar Mahundi (wa pili).
 Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja baina ya Wajasiriamali Wadogo wa Usindikaji wa Vyakula mkoani Katavi, Watumishi wa TFDA, na wawezeshaji kutoka Taasisi za Serikali katika Ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili, tarehe 2 – 3 Julai 2018 katika Ukumbi wa Mkutano wa Idara ya Maji katika Halmashauri ya Mpanda.
Mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya Mpanda, Bi. Enelia Lutungulu (aliyesimama) akiwasilisha hotuba ya kufunga mafunzo ya Wajasiriamali Wadogo wa Usindikaji wa Vyakula mkoani Katavi (hawapo pichani) yaliyofanyika tarehe 2 – 3 Julai 2018 katika Ukumbi wa Mkutano wa Idara ya Maji, Halmashauri ya Mpanda. Waliokaa kutoka kulia, ni Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka TFDA, Bw. Justin Makisi na Meneja wa TFDA Kanda ya Magharibi, Dkt. Edgar Mahundi (wa pili).

Na James Ndege - Katavi
TFDA imeendesha mafunzo ya siku mbili kwa wajasiriamali wadogo wa usindikaji wa vyakula mkoani Katavi ikiwa ni mojawapo ya mikakati yake ya kuwezesha ukuaji wa Sekta ya  viwanda nchini. Mafunzo yamehusisha wajasiriamali 120 wa mkoa wa Katavi  hayo kuanzia tarehe 2 – 3 Julai 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mpanda uliopo mjini Mpanda.

Mafunzo hayo yalifunguliwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Huruma I. Mwalutanile aliwaasa washiriki kutumia fursa hiyo kwa ukamilifu ili waweze kukidhi vigezo muhimu vya kisheria na kuzalisha bidhaa bora, salama na zenye ufanisi ili kukidhi soko la ndani na nje ya nchi jambo litakalochangia ukuaji wa uchumi wa nchi lakini pia kulinda afya ya jamii kwa kuwa TFDA ipo karibu na kundi hili muhimu katika uanzishaji wa viwanda nchini kwa kutatua changamoto zao.

“Ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini kutatua changamoto zinazowakabili katika usajili wa majengo na bidhaa zao, uongozi wa mkoa kupitia halmashauri zake umeanza kutenga maeneo maalum ya wajasiriamali kuzalishia bidhaa zao”, Kaimu Katibu Tawala huyo alisisitiza.


Hivyo makala TFDA YAWEZESHA MKOA WA KATAVI KUWA NA VIWANDA VINGI VYA UZALISHAJI VYAKULA

yaani makala yote TFDA YAWEZESHA MKOA WA KATAVI KUWA NA VIWANDA VINGI VYA UZALISHAJI VYAKULA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TFDA YAWEZESHA MKOA WA KATAVI KUWA NA VIWANDA VINGI VYA UZALISHAJI VYAKULA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tfda-yawezesha-mkoa-wa-katavi-kuwa-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TFDA YAWEZESHA MKOA WA KATAVI KUWA NA VIWANDA VINGI VYA UZALISHAJI VYAKULA"

Post a Comment