title : TBA YAJIPANGA KUOKOA MABILIONI KATIKA MIRADI YA UJENZI
kiungo : TBA YAJIPANGA KUOKOA MABILIONI KATIKA MIRADI YA UJENZI
TBA YAJIPANGA KUOKOA MABILIONI KATIKA MIRADI YA UJENZI
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jmaii
WAKALA wa Majengo Tanzania(TBA), limesema imejipanga kuokoa mabilioni ya fedha za miradi hapa nchini ambapo itatekeleza miradi 180 ambayo itagharimu Sh billion 350.
Akizungumza katika maonesho 42 ya Biashara ya kimataifa yanayofanyika katika Viwanja Vya mwalimu Nyerere Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga amesema gharama hizo ni nafuu ambapo ingetekelezwa na waty wengine ingekuwa kubwa zaidi.
Alisema mpaka sasa wanajivunia kutekeleza miradi saba ambayo ni pamoja na mradi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ambao umegharimu Sh.billioni 10 ambapo wameweza kuokoa billioni 80 endapo mradi huo ungetekelezwa na wakandarasi wengine.
Amesema kwa mradi wa ujenzi hospitali ya Geita wameweza kuokoa billioni 75 na wamejenga kwa billioni 17.
Pia mradi wa hospitali ya Wilaya ya Chato wameokoa Sh.Billioni 60 na wamejenga kwa billioni 13
Katika ujenzi wa Nyumba za magomeni Jijini Dar es salaam wameokoa sh billioni 86 na ujenzi utagalimilu billioni 20.
Mwakalinga alisema TBA inajivunia kuwa na rasilimali watu iliyo bora ambapo mpaka sasa inawataalamu 83 wahandisi 73 pamoja na wabunifu majengo 10.
"Tunajivunia rasilimali watu tulizonazo...ambao ni wazalendo na ndio maana tunajivunia ujenzi ulio bora " alisema Mwakalinga.
Amesema katika mwaka 2017 /2018 uliomalizika mwezi Juni TBA imetoa asilimia 15,ya mapato taluopatikana katika miradi yao ambao ni billioni 2 na kuzipeleka hazina.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch.Elius Mwakalinga akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana uokoaji nwa fedha miradi mbalimbali wakati alipotembelea banda TBA katika maonesho 42 ya Biashara ya kimataifa yanayofanyika katika Viwanja Vya mwalimu Nyerere.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch.Elius Mwakalinga akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wakala huo TBA katika maonesho 42 ya Biashara ya kimataifa yanayofanyika katika Viwanja Vya mwalimu Nyerere.
Mteja akipata maelezo ya katika banda la TBA alipotembelea banda TBA katika maonesho 42 ya Biashara ya kimataifa yanayofanyika katika Viwanja Vya mwalimu Nyerere
Hivyo makala TBA YAJIPANGA KUOKOA MABILIONI KATIKA MIRADI YA UJENZI
yaani makala yote TBA YAJIPANGA KUOKOA MABILIONI KATIKA MIRADI YA UJENZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TBA YAJIPANGA KUOKOA MABILIONI KATIKA MIRADI YA UJENZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tba-yajipanga-kuokoa-mabilioni-katika.html
0 Response to "TBA YAJIPANGA KUOKOA MABILIONI KATIKA MIRADI YA UJENZI"
Post a Comment