title : VETA YAJIPANGA KUTOA UJUZI KATIKA SEKTA YA VIWANDA
kiungo : VETA YAJIPANGA KUTOA UJUZI KATIKA SEKTA YA VIWANDA
VETA YAJIPANGA KUTOA UJUZI KATIKA SEKTA YA VIWANDA
Na Chalila Kibuda Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) imesema kuwa wamejipanga katika utoaji wa elimu ufundi katika uchumi wa viwanda.
Akizungumza mara baada ya kupokoea kikombe cha ushindi Mwenyekiti wa bodi ya VETA, Peter Maduki amesema kuwa dhamira ya VETA ni kuhakikisha viwanda vinapata ujuzi unaotoka VETA.
Amesema kuwa kumekuwa na mafanikio katika utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi ikiwa nipamoja vijana kuingia katika soko la ajira za moja kwa moja na wengine wakijiajiri .
Maduki amesema katika uchumi wa viwanda VETA ina nafasi kubwa hivyo ni wajibu wao kuzalisha vijana wengi wa kutumika katika uchumi huo na taifa kusonga mbele .
Aidha ametoa wito wa vijana kujiunga na vyuo vya VETA katika kupata ujuzi na kuwa watu kuzalisha pamoja na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.
“Hatutarudi nyuma kwa kuliacha jambo la viwanda wakati ni sehemu ya wadau muhimu wa katika utoaji wa ujuzi wa viwanda”
Wafanyakazi wa VETA wakiwa katika furaha ya ushindi wa kikombe katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
.Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano Watanzania, Kassim Majaliwa akikabidhi kikombe cha ushindi kwa Mwenyekiti wa Bodi wa VETA, Peter Maduki katika ufunguzi wa maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa VETA kipawa akitoa maelezo ya ubunifu wa uzio wa ulinzi kwa mwananchi aliyepotembelea banda katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala VETA YAJIPANGA KUTOA UJUZI KATIKA SEKTA YA VIWANDA
yaani makala yote VETA YAJIPANGA KUTOA UJUZI KATIKA SEKTA YA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VETA YAJIPANGA KUTOA UJUZI KATIKA SEKTA YA VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/veta-yajipanga-kutoa-ujuzi-katika-sekta.html
0 Response to "VETA YAJIPANGA KUTOA UJUZI KATIKA SEKTA YA VIWANDA"
Post a Comment