title : MANISPAA YA TEMEKE YAHUDUMIA WANANCHI MSIMU WA SABASABA
kiungo : MANISPAA YA TEMEKE YAHUDUMIA WANANCHI MSIMU WA SABASABA
MANISPAA YA TEMEKE YAHUDUMIA WANANCHI MSIMU WA SABASABA
Na Zainab Nyamka,Glogu ya jamii
HALMASHAURI ya Manispaa ya Temeke imepiga kambi katika viwanja vya sabasaba ikiwa na lengo maalumu la kuwahudumia wananchi katika msimu wa sabasaba na kuwataka wakazi wa Temeke wajitokeze kwa wingi ukizingatia maonesho hayo yanafanyika katika Manispaa yao.
Akizungumza na blogu ya jamii Afisa biashara wa Manispaa ya Temeke bi. Telphina Mbegu ameeleza kuwa katika msimu huu wa sabasaba wanatoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na leseni za biashara kwa wateja wapya na kwa wateja ambao leseni zao zimeisha muda wake wa matumizi.
Aidha ameeleza kuwa wanatoa leseni mbalimbali kama na ushauri kama taratibu za ujenzi makazi, vileo na huduma mbalimbali za kibiashara.
Pia ameeleza kuwa kama Manispaa wanasikiliza kero na maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi na kutatua kero hizo zinazowakabili wananchi wa Manispaa hiyo.
Kuhusiana na kero walizopokea Mbegu ameeleza kuwa wananchi wengi wametoa kero kuhusiana na miundombinu hasa ya barabara, mifereji na takataka katika maeneo mbalimbali katika maeneo wanayoishi.
Pia ameeleza kuwa wanatoa elimu kwa wafanyabiashara wanaotaka kuanza biashara kwa kutoa elimu kuhusiana na upataji wa leseni kwa ajili ya biashara hizo.
Amewaomba wakazi wa Temeke na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ili waweze kujifunza na kuelimika zaidi kupitia shughuli zinazofanywa na Manispaa hiyo.
Afisa biashara wa Manispaa ya Temeke Telphina Mbegu akielezea huduma wanazozitoa katika banda liliopo ndani ya Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Afisa biashara wa Manispaa ya Temeke Telphina Mbegu akimuelezea Jambo mwananchi aliyetembelea banda lao ndani ya Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala MANISPAA YA TEMEKE YAHUDUMIA WANANCHI MSIMU WA SABASABA
yaani makala yote MANISPAA YA TEMEKE YAHUDUMIA WANANCHI MSIMU WA SABASABA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MANISPAA YA TEMEKE YAHUDUMIA WANANCHI MSIMU WA SABASABA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/manispaa-ya-temeke-yahudumia-wananchi.html
0 Response to "MANISPAA YA TEMEKE YAHUDUMIA WANANCHI MSIMU WA SABASABA"
Post a Comment