TAMASHA LA (TANZANIA-CHINA CULTURE FESTIVAL)LAFANYIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

TAMASHA LA (TANZANIA-CHINA CULTURE FESTIVAL)LAFANYIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAMASHA LA (TANZANIA-CHINA CULTURE FESTIVAL)LAFANYIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAMASHA LA (TANZANIA-CHINA CULTURE FESTIVAL)LAFANYIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM
kiungo : TAMASHA LA (TANZANIA-CHINA CULTURE FESTIVAL)LAFANYIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

soma pia


TAMASHA LA (TANZANIA-CHINA CULTURE FESTIVAL)LAFANYIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

MKUU wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika Tamasha la Tanzania na China Festival lililofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho Posta jijini Dar es salaam jana na kuhudhuriwa na wananchi watanzania pamoja na wananchi wa China waishio nchini Tanzania ili kukuza uhusiano na Urafiki katika kupitia Utamaduni na Sanaa.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza wakati akiakipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei katika Tamasha la Tanzania na China Festival lililofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho Posta jijini Dar es salaam jana
Katibu wa Chama cha kukuza uhusiano wa Tanzania na china Joseph Kahama akizungumza katika tamasha hilo lililofanyika jana jijini Dar es salaam.

Balozi mpya wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi Wang Ke akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema kushoto na Katibu wa Chama cha kukuza uhusiano wa Tanzania na china Joseph Kahama na Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Weiwa pili kutoka kulia.
Baadhi ya raia wa China waishio nchini Tanzania wakiwa katika tamasha hilo.




Kikundi cha muziki chenye mchanganyiko wa Wanzania na Wachina kikiimba nyimbo katika tmasha hilo. Baadhi ya Madaktari kutoka nchini China ambao wametoa huduma za matibabu katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania wakiimba wimbo maalum katika tamasha hilo.




Burudani kutoka China zikiendelea


Waimbaji kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakiimba katika tamasha hilo.



Wageni mbalimbali walioalikwa katika tamasha hilo.

MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema ipo haja ya kuendelea kuudumisha uhusuiano kati ya Tanzania na China kwani una faida nyingi na wenye mambo yanayofanana.

Amesema kuwa Tanzania na china zimekuwa na uhusiano wa kaka na dada na msingi wake mkubwa uliwekwa na waasisi wa nchi hizo mbili ambapo kwa Tanzania ni Hayati Mwalimu Julius Nyerere na China Mao Se tung.

Mjema aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa Tamasha la burudani lililowahusisha watanzania na wachina waishio nchini Tanzania ambalo lilifanyika ukumi wa Makumbusho ya Taifa

Tamasha hilo limeandaliwa na Chama cha kukuza uhusiano wa Tanzania na China (TANZANIA- CHINA FRIENDSHIP PROMOTION ASSOCIATION) ambapo Mjema amepongeza Chama hicho kwa uamuzi wake wa kuandaa tamasha hilo kwa lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo.

" Wakati tunapata uhuru Tanzania na china kuna mambo mengi yanafanana yakiwemo ya burudani kwa maana utamaduni " alisema

Pia alisema ubalozi wa china nchini Tanzania kupitia Balozi wake Wang ke umedhihirisha namna wanavyotambua na kuenzi utamaduni baina ya nchi hizo mbili kwani ndio waliodhamini tamasha hilo.

Hata hivyo Mjema na balozi Wang Ke pamoja na wageni waalikwa walipata nafasi ya kuangalia burudani huku nyimbo maalumu ya kuzungumzia uhusiano wa china na Tanzania ukiwagusa waliohudhuria Tamasha hilo.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha kukuza uhusiano wa Tanzania na china Joseph Kahama alisema tamasha hilo ambaloni kwa mara ya kwaza limefanyika nchini Tanzania lengo haswa nikusaidia uelewa kati ya watu na watu.

Alifafanua kuwa linalenga kufahamiana zaidi na kuendeleza undugu ambao upo kati ya Tanzania na watu wa china na hilo ndio lengo kubwa na ndio maana hata nyimbo wanaimba pamoja kati ya wachina na watanzania.

Kahama alisema tamasha hilo ambalo limepewa jina la (Tanzania - China Culture Ferstival) litaendelea kuimarisha na kudumisha uhusiano mzuri na kwa hapa nchini linafanyika kwa mara ya kwaza na litakuwa linafanyika kila mwaka na watakuwa wanafanya maboresho kadri watakavyokuwa wanafanya.


Hivyo makala TAMASHA LA (TANZANIA-CHINA CULTURE FESTIVAL)LAFANYIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

yaani makala yote TAMASHA LA (TANZANIA-CHINA CULTURE FESTIVAL)LAFANYIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAMASHA LA (TANZANIA-CHINA CULTURE FESTIVAL)LAFANYIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tamasha-la-tanzania-china-culture_93.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAMASHA LA (TANZANIA-CHINA CULTURE FESTIVAL)LAFANYIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM"

Post a Comment