TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar

TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar
kiungo : TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar

soma pia


TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar

TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018, limefunguliwa juzi usiku huku Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikijipiga kifua kusaidia utatuzi wa changamoto zinazoikabili tasnia ya filamu nchini. 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa tamasha hilo la 21 katika ukumbi wa Ngome Kongwe mjini Zanzibar, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi, alikiri kuwa pamoja na mafanikio yake, kuna maeneo ambayo halijafanya vizuri.

Alisema miongoni mwa upungufu huo, ni kutokufikiwa ufanisi wa asilimia 100 katika ulinzi wa haki za wabunifu na watengenezaji filamu, akisema iko haja ya kuuangalia upande huo kwa jicho la tatu ili wasanii hao wafaidi matunda ya jasho lao.

Aliiambia hadhira iliyofurika ukumbini hapo wakiwemo watalii kutoka nchi mbalimbali, kuwa Serikali ya Zanzibar ilianzisha kwa nia njema Ofisi ya Msimamizi wa Haki za Ubunifu (COSOZA), mfumo unaoendeshwa kimataifa ili kulinda haki za wasanii.

Alifahamisha kuwa tasnia ya filamu ni miongoni mwa maeneo yanayoweza kusaidia kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kijamii hasa uhaba wa ajira, kama ilivyo katika mataifa mengine yaliyopiga hatua kubwa kifilamu na matamasha yanayotambulika kimataifa.

“Kwa upande wa serikali, naamini taasisi na vyombo husika vitaendelea kusimamia upatikanaji wa haki kwa waliopoteza jasho lao katika tasnia hii ili nao wanufaike kwa malengo waliyojiwekea,” alisema.Waziri huyo alisema kuanzishwa kwa COSOZA ni sehemu ya msukumo wa serikali katika kutoa mchango ili kuwainua kimaisha wananchi waliojikita katika tasnia ya filamu.


 Baadhi ya vikundi mbalimbali pichani juu na chini vikiwasili kwenye uzinduzi wa tamasha hilo la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018.


Hivyo makala TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar

yaani makala yote TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tamasha-la-kimataifa-la-filamu-zanzibar.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar"

Post a Comment