title : TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUZINDUA HUDUMA MPYA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI RUVUMA
kiungo : TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUZINDUA HUDUMA MPYA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI RUVUMA
TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUZINDUA HUDUMA MPYA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI RUVUMA

Kuanzishwa kwa huduma hii kutasaidia wananchi wengi hasa wa mikoani ambako ni mbali na Taasisi yetu ilipo kufikiwa kwa urahisi zaidi na kupata huduma za matibabu ya moyo ya kibingwa.
Baada ya kufanyika kwa uzinduzi huo tutaendelea kutoa huduma kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa muda wa siku sita kuanzia tarehe 23-28/7/2018. Huduma hii ya kliniki inayotembea itakuwa endelevu katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Siku za karibuni tutatoa ratiba kamili kadri ya maombi yatakavyotufikia kutoka Tawala za Mikoa.
Huduma tutakazozitoa ni kutoa matibabu baada ya kufanya vipimo kwa kutumia mitambo mahususi tuliyokuwa nayo. Ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, elimu ya lishe bora, kutoa Rufaa ya moja kwa moja kwa wagonjwa watakaokutwa na matatizo ya Moyo kuja kwenye Taasisi yetu kwa uchunguzi wa tiba zaidi.
Dhumuni la Taasisi ni kuhakikisha kila mgonjwa anapata huduma bora na kuwa na elimu inayohusiana na magonjwa ya Moyo. Wananchi wote wa mkoa wa Ruvuma pamoja na mikoa ya jirani tunawakaribisha mfike katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma (Songea) ili muweze kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
Hivyo makala TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUZINDUA HUDUMA MPYA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI RUVUMA
yaani makala yote TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUZINDUA HUDUMA MPYA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI RUVUMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUZINDUA HUDUMA MPYA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI RUVUMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/taasisi-ya-moyo-jakaya-kikwete-kuzindua.html
0 Response to "TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUZINDUA HUDUMA MPYA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI RUVUMA"
Post a Comment