title : SHULE YA SEKONDARI YA KISIMIRI YAPONGEZWA KWA KUSHIKA NAFASI PILI KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA SITA
kiungo : SHULE YA SEKONDARI YA KISIMIRI YAPONGEZWA KWA KUSHIKA NAFASI PILI KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA SITA
SHULE YA SEKONDARI YA KISIMIRI YAPONGEZWA KWA KUSHIKA NAFASI PILI KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA SITA
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha Christopher Kazeri amewapongeza walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri kwa kufanikisha kushika nafasi ya pili kitaifa matokeo ya mtihani wa kidato cha sita.
Nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani imeshikwa na Shule ya Sekondari Kibaha kati ya shule 543 zilizofanya mtihani huo.Akizungumza leo wakati akitoa pongezi hizo Kazeri amesema walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri kwa jitihada zao wamefanikisha shule hiyo kushika nafasi ya pili kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka huu 2018.
Pia amewataka walimu hao kuongeza bidii katika ufundishaji ili kupata matokeo mazuri zaidi kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mitihani ijayo.Akiwa shuleni hapo pamoja na kutoa pongezi kwa walimu, wazazi na wanafunzi amepata nafasi ya kusikiliza na kutatuo changamoto zinazowakabili walimu kwa lengo la kuleta tija zaidi kwenye taaluma ya Shule hiyo.
Kwa upande wa Makamu Mkuu wa shule ya Sekondari Kisimiri Mwalimu John Awe amesema kuwa mojawapo ya mbinu zilizotumika kuhakikisha shule hiyo inapata matokeo mazuri illikuwa kutoa mafunzo ya ziada kwa wanafunzi waliokuwa na uwezo mdogo.
"Hivyo walimu walitenga muda wa ziada kuwafundisha wanafunzi hao ambao wengi wao walifanya vibaya kwenye mtihani wa utamirifu (MOCK) kwa kupata alama sifuri,"amesema.
Pia amesema walimu wa shule hiyo wana moyo wa kufundisha na kufafanua kwenda darasani ni suala moja na kufundisha kama inavyotakiwa na wanafunzi kuelewa ni jambo jingine .
Wakati walimu nao walimu wametoa changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwamo ya uhaba wa viti vya walimu 50 na madawati ya wanafunzi 300.Pi walimu hao wamehitaji ufafanuzi wa maslai yao kama watumishi ikiwemo kupanda daraja.Akitoa ufafanuzi wa masuala ya watumishi Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Grace Mbilinyi amesema kutokana na mchakato wa kuwabaini watumishi hewa na wenye vyeti vya kugushi Serikali ilisitasha upandaji madara kwa watumishi wa umma.
"Ila kwa sasa maelekezo mbalimbali yanatolewa.Kuhusu malipo ya likizo ni vema walimu mkaweka viambatanisho vyote muhimu vikiwemo vyeti vya watoto vya kuzaliwa na vyeti vya ndoa,"amesema.Aidha katika matokeo haya ya shule ya Sekondari Kisimiri imeonesha kuweka rekodi nzuri ya kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani hiyo ya kidato cha sita.
"Kwani kwa miaka 3 mfululizo imekuwa kwenye kundi la shule tatu bora kitaifa.Mwaka 2016 ilishika nafasi ya kwanza, mwaka 2017 ikashika nafasi ya tatu na kwa mwaka huu 2018 imeshika nafasi ya pili kitaifa."Kwa watahiniwa wetu 67 kupata daraja la kwanza na la pili ikiwa 51 kati yao wamepata daraja la kwanza na 16 kupata daraja la pili,"amefafanua.
Imeelezwa matokeo ya Sekondari ya Kisimiri imezidi kuutangaza mkoa wa Arusha wenye shule 31 zenye watahiniwa zaidi ya 30 za Serikali na binafsi.
Hivyo makala SHULE YA SEKONDARI YA KISIMIRI YAPONGEZWA KWA KUSHIKA NAFASI PILI KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA SITA
yaani makala yote SHULE YA SEKONDARI YA KISIMIRI YAPONGEZWA KWA KUSHIKA NAFASI PILI KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA SITA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHULE YA SEKONDARI YA KISIMIRI YAPONGEZWA KWA KUSHIKA NAFASI PILI KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA SITA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/shule-ya-sekondari-ya-kisimiri.html
0 Response to "SHULE YA SEKONDARI YA KISIMIRI YAPONGEZWA KWA KUSHIKA NAFASI PILI KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA SITA"
Post a Comment