title : SERIKALI YAONDOA RIBA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU
kiungo : SERIKALI YAONDOA RIBA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU
SERIKALI YAONDOA RIBA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU
Na WAMJW CHATO - GEITA
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza rasmi kuwa hakutakuwa na riba katika mikopo itakayotolewa kwa wanawake, vijana na walemavu katika ngazi ya Halmashauri.
Kauli hiyo imetolewa wilayani Chato na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokitembelea kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Jikomboe.
Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kuwasaidia Wanawake, vijana na walemavu kujikwamua kiuchumi hivyo imeona ni bora mikopo itolewe bila riba ili kuwapa fursa wanawake, vijana na walemavu kwa ajili ya kuanzisha miradi ya wingi ya kujikwamua kiuchumi.
Ameongeza kuwa suala la riba limekuwa kikwazo kwa makundi mengi kuweza kukopa na kurejesha mikopo kwa wakati.
"Niseme tu tumeliangalia suala hili kwa karibu ili tuwawezeshe wananchi hasa wanawake, vijana na walemavu kujikwamua kiuchumi" alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Mbunge wa Chato (CCM) na Waziri wa Madini Dkt. Medard Kalemani akimshukuru Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kwa ziara yake alioyoifanya katika kata za wilaya ya Chato mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya Naibu Waziri huyo ya siku mbili mkoani humo.
Mwekahazina wa kikundi cha Jikomboe kilichopo wilayani Chato Mkoani Geita akiwasilisha risala yao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wkati wa kuhitimishwa kwa ziara yake alioyoifanya katika kata za wilaya ya Chato mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya Naibu Waziri huyo ya siku mbili mkoani humo.
Baadhi ya wananawake wajasiriamali wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akihitimisha ziara yake alioyoifanya katika kata za wilaya ya Chato mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri huyo mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia malighafi inayotumika kutengeneza batiki wakati alipokitembelea kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Jikomboe kilichopo Wilaya ya Chato wakati akihitimishaziara yake alioyoifanya katika kata za wilaya ya Chato mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya siku mbiliua Naibu Waziri huyo mkoani humo.
Hivyo makala SERIKALI YAONDOA RIBA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU
yaani makala yote SERIKALI YAONDOA RIBA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAONDOA RIBA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/serikali-yaondoa-riba-mikopo-ya_28.html
0 Response to "SERIKALI YAONDOA RIBA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU"
Post a Comment