title : SEKTA BINAFSI,POLISI,IDARA YA MAHAKAMA ZADAIWA KUONGOZA KULALAMIKIWA KWA VITENDO VYA RUSHWA
kiungo : SEKTA BINAFSI,POLISI,IDARA YA MAHAKAMA ZADAIWA KUONGOZA KULALAMIKIWA KWA VITENDO VYA RUSHWA
SEKTA BINAFSI,POLISI,IDARA YA MAHAKAMA ZADAIWA KUONGOZA KULALAMIKIWA KWA VITENDO VYA RUSHWA
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Ilala imesema taasisi za idara ya sekta binafsi, polisi na idara ya mahakama ndizo zinazoongoza kulalamikiwa zaidi kwa vitendo vya rushwa.
Amezitaja pia Tamisemi, Idara ya Afya, Wizara ya Ardhi, idara ya elimu na kampuni za bima.
Zainabu Bakari ambaye ni mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala,amesema hayo Leo Julai 31 ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya utendaji wao wa kazi kwa mwaka 2017/2018.
Amesema, katika kipindi hicho chote walichokitaja, Takukuru imeweza kupokea taarifa za rushwa 352 kwa njia mbali mbali zikiwamo njia za simu, barua na watu kufika ofisini.Amesema kutokana na taarifa hizo, majalada 25 yamefunguliwa na yana RB huku majalada 15 yakiwa tayari yamekamikika na majalada saba yamepokelewa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kuombewa kibali cha mashtaka.
Ameongeza kuwa, ni majalada manne tu ndio yamepata kibali cha DPP, na kesi mpya 12 zimeishafunguliwa mahakamani huku kesi walizoshinda zikiwa saba na kesi walizoshindwa ni tano.Zainabu ameeleza kuwa, Takukuru wanafanya udhibiti wa rushwa kwa kufanya uchambuzi wa mifumo na ufuatiliaji wa fedha za miradi ya maendeleo ili kubaini mianya ya rushwa iliyopo katika taasisi na idara mbali mbali na katika matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.
Aidha ameshauri wakandarasi walipwe kwa wakati ili kumaliza tatizo la rushwa na kusema katika kipindi hiki wamefuatilia matumizi ya fedha ya maendeleo kwa uratibu wa Public Expenditure Trucking Survey(PETS) kwa idara za ujenzi na maji na kubaini kuwepo kwa ucheleweshaji wa maalipo ya wakandarasi.
Amewaasa Mwananchi pale wanapoona kuna dalili ama ushawishi wa rushwa mahali popote wasisite kutoa taarifa takukuru kwa kuwa rushwa ni adui wa haki na maendeleo.
Hivyo makala SEKTA BINAFSI,POLISI,IDARA YA MAHAKAMA ZADAIWA KUONGOZA KULALAMIKIWA KWA VITENDO VYA RUSHWA
yaani makala yote SEKTA BINAFSI,POLISI,IDARA YA MAHAKAMA ZADAIWA KUONGOZA KULALAMIKIWA KWA VITENDO VYA RUSHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SEKTA BINAFSI,POLISI,IDARA YA MAHAKAMA ZADAIWA KUONGOZA KULALAMIKIWA KWA VITENDO VYA RUSHWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/sekta-binafsipolisiidara-ya-mahakama.html
0 Response to "SEKTA BINAFSI,POLISI,IDARA YA MAHAKAMA ZADAIWA KUONGOZA KULALAMIKIWA KWA VITENDO VYA RUSHWA"
Post a Comment