title : RC KIGOMA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA, WAHANDISI KUUSIMAMIA MRADI WA MAJI MUHANGE
kiungo : RC KIGOMA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA, WAHANDISI KUUSIMAMIA MRADI WA MAJI MUHANGE
RC KIGOMA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA, WAHANDISI KUUSIMAMIA MRADI WA MAJI MUHANGE
Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emanueli Maganga amewaagiza wakuu wa wilaya za Kibondo na Kakonko pamoja na Wahandisi wa Wilaya hizo kuweka kambi katika Kata ya Muhange kuhakikisha wanasimamia mradi wa maji wa Muhange unatoa maji kwa wananchi ndani ya wiki mbili.
Kauli hiyo aliitoa wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya miradi ya maji ndani ya Wilaya ya Kakonko ambapo amesikitishwa na kitendo cha mradi wa maji Muhange kutokamilika licha ya kwamba ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2012 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia na ulitarajiwa kukamilika Desemba mwaka 2013.
Brigedia Maganga amesema ni jambo la kushangaza kuona wananchi wanaendelea kupata shida ya maji huku mradi ukiwa umefungwa kwa changamoto ndogondogo ambazo zinaweza kufanyiwa marekebisho na ukizingatia mradi huo unasimamiwa na Wilaya mbili na Wahandisi wawili.
Hivyo amewataka kutenga muda wa siku mbili kufika katika Kijiji cha Muhange kushirikiana na wananchi kukamilisha mapungufu ya mradi huo.
"Ukiwa Mhandisi kazi yako ni kukaa sehemu ya mradi hadi mradi utakapo kamilika, kama mngekuja kukaa hapa changamoto hizi zisingejitokeza mme waachia wakandarasi wafanye mradi kwa kiwango cha chini, wananchi wanapampu maji yana ishia chini na haya wafikii na wananchi wanaendelea kuteseka", amesema Brigedia Maganga.
Ameongeza kuwa " Wakuu wote wa wilaya mbili kaeni na hii kamati ya watumia Maji na wataalamu wenu mje hapa na Jumuiya ya Watumia maji kama tatizo la mabomba mtafute maeneo yanayo vuja yafanyiwe ukarabati kama kuna tatizo la kisiasa litajulikana suala ni kwenye utendaji na utekelezaji mpaka maji yaende kwenye gati zote 24 wananchi wapate maji".
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emanueli Maganga akizungumza na baadhi ya viongozi wakiwemo wakuu wa wilaya za Kibondo na Kakonko pamoja na Wahandisi wa Wilaya hizo kuweka kambi katika Kata ya Muhange kuhakikisha wanasimamia mradi wa maji wa Muhange unatoa maji kwa wananchi ndani ya wiki mbili.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga katikati akioneshwa moja ya tanki la maji na Muhandisi Michael Nguruwe (kushoto),katika Katika Kata ya Nyagwijima wilayani Kakonko Mkoani Kigoma Jana,pichani kulia ni Muhandisi Elinatha Elisha.
Hivyo makala RC KIGOMA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA, WAHANDISI KUUSIMAMIA MRADI WA MAJI MUHANGE
yaani makala yote RC KIGOMA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA, WAHANDISI KUUSIMAMIA MRADI WA MAJI MUHANGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC KIGOMA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA, WAHANDISI KUUSIMAMIA MRADI WA MAJI MUHANGE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/rc-kigoma-atoa-maagizo-kwa-wakuu-wa.html
0 Response to "RC KIGOMA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA, WAHANDISI KUUSIMAMIA MRADI WA MAJI MUHANGE"
Post a Comment