title : PROGRAMU YA 'UNI LIFE CAMPUS' YAFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA
kiungo : PROGRAMU YA 'UNI LIFE CAMPUS' YAFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA
PROGRAMU YA 'UNI LIFE CAMPUS' YAFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania waaswa kuzilinda na kuzitunza fursa wanazozipata ili ziweze kuwaletea maendeleo endelevu katika maisha yao. Hayo yamesemwa na Mwanzilishi wa programu ya 'Uni Life Campus' Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Esther Mmasi ambaye anawakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita katika semina elekezi ya kuwaasa wanafunzi waliopata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo (field) katika tasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi.
"Nawaomba sana wanavyuo wenzangu huko mnapokwenda mkawe mabalozi wema, mzingatie kuwa watiifu na muwe na moyo wa kujifunza huku mkifanya kazi kwa bidii hapo mnaweza kupata maarifa mapya," amesema Mhe. Esther Mmasi. Amesema kuwa tatizo la vijana wengi kwa sasa wamekuwa ni wakaidi na wanaoendeleza uvivu huku simu ikiwa ni kikwazo kikubwa pindi wanapofanya kazi.
"Mkienda kwenye mafunzo kwa vitendo (field) mzingatie kufanya kazi na si kushinda unachezea simu maana wengi wenu kutwa kucha ni kuchat tu unasahau hata kilichowapeleka katika ofisi za watu, nangoja ripoti njema zitakazowajenga mbeleni" Amesema.
Aidha amesema kuwa mpka sasa Programu ya 'Uni Life Campus' imewatafutia nafasi za mafunzo kwa vitendo (field) wanafunzi wapatao 100 waliokuwa wameomba kutoka vyuo mbali mbali Tanzania na watakwenda Shirika la Taifa la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Benki ya NMB na Benki ya Posta Tanzania (TPB).
"Tunamshukuru Mungu tumeweza kuwatolea changamoto wanafunzi hasa waliokuwa wakiomba mafunzo kwa vitendo, tulipotangaza mwaka jana mwishoni zaidi ya vijana 1,900 waliweza kuomba ila tumeweza wapatia nafasi 100 ambao tulizipata licha ya kuendelea kuongea na taasisi mbali mbali za serikali ambazo zimetuahidi kutupatia nafasi zaidi ya 600," amesema.
Mwanzilishi wa programu ya 'Uni Life Campus' Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Esther Mmasi ambaye anawakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbali mbali vya Tanzania wakati wa semina elekezi juu ya kuzitunza fursa wanazozipata katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kupatiwa nafasi za kufanya mafunzo kwa vitendo (field) katika taasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi mwishoni mwa wiki iliyopita katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam. Picha zote na Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Mkurugenzi DM Saikolojia Limited Bw. Dosi Said Dosi akitoa neno kwa wanafunzi wanaotarajia kuanza mafunzo yao kwa vitendo (field) wakati wa semina elekezi juu ya kuzitunza fursa wanazozipata katika maisha yao katika taasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi mwishoni mwa wiki iliyopita katika Chuo cha CBE jijini Dar es Salaam..
Mmoja ya maofisa katika Programu ya 'Uni Life Campus' Gladness akitoa maelezo machache kwa wanafunzi.
Hivyo makala PROGRAMU YA 'UNI LIFE CAMPUS' YAFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA
yaani makala yote PROGRAMU YA 'UNI LIFE CAMPUS' YAFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROGRAMU YA 'UNI LIFE CAMPUS' YAFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/programu-ya-uni-life-campus-yafanikisha.html
0 Response to "PROGRAMU YA 'UNI LIFE CAMPUS' YAFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA"
Post a Comment