title : NHIF KAGERA WATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA KITUO CHA KULELEA WAZEE.
kiungo : NHIF KAGERA WATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA KITUO CHA KULELEA WAZEE.
NHIF KAGERA WATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA KITUO CHA KULELEA WAZEE.
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera
MFUKO wa Taifa wa Bima ya afya(NHIF) Mkoa wa Kagera wamekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wanaosaidia wazee katika kituo cha kulelea wazee cha kilima kilichopo halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.
Meneja wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Kagera Elias Odhiambo alisema kuwa huo ni utekelezaji wa ahadi ilitolewa na mfuko katika harambee ya kuchangisha fedha na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi kwenye kituo cha kulelea wazee cha kiilima ambazo ziliathiriwa na tetemeko la ardhi ambapo harambee hiyo iliendeshwa na Naibu Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia na watoto Faustine Andungulile.
"NHIF leo tumetimiza ahadi yetu tuliyotoa ya kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi kwaajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika kituo hiki,hii ni sehemu ya misaada inayotolewa na mfuko kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo,naamini msaada huu utasaidia ujenzi wa makazi haya"alisema
Odhiambo alisema vifaa walivyokabidhi ni mifuko 100 ya sementi na mabati 50 vifaa hivyo vyote vinathamani ya shilingi 3,100,000.Baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu aliushukuru uongozi wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)kwa kutimiza ahadi yao waliyo haidi kwa wakati.
"Meneja ninakuomba nifikishie shukrani zangu kwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko mmetekeleza ahadi yenu mliyotoa ndani ya wakati ili kufanikisha zoezi hili la ujenzi"alisema.Kijuu aliwataka wakandarasi kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa kasi na kukamilika kwa wakati aliwaomba pia wadau wengine kuendelea kutoa misaada ili ujenzi huo uweze kukamilika.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akipokea vifaa vya ujenzi ikiwemo saluji na mabati kutoka kwa Meneja wa mfuko wa bima ya afya (NHIF) Kagera Elias Odhiambo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Kulelea Wazee
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiwasalimia baaddhi ya Wazee walioko kwenye kituo chao
Sehemu ya ujenzi wa kituo hicho ukiendelea
Hivyo makala NHIF KAGERA WATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA KITUO CHA KULELEA WAZEE.
yaani makala yote NHIF KAGERA WATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA KITUO CHA KULELEA WAZEE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NHIF KAGERA WATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA KITUO CHA KULELEA WAZEE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/nhif-kagera-watoa-msaada-wa-vifaa-vya.html
0 Response to "NHIF KAGERA WATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA KITUO CHA KULELEA WAZEE."
Post a Comment