Naibu Waziri kubariki Tamasha la nywele, ngozi za asili

Naibu Waziri kubariki Tamasha la nywele, ngozi za asili - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Naibu Waziri kubariki Tamasha la nywele, ngozi za asili, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Naibu Waziri kubariki Tamasha la nywele, ngozi za asili
kiungo : Naibu Waziri kubariki Tamasha la nywele, ngozi za asili

soma pia


Naibu Waziri kubariki Tamasha la nywele, ngozi za asili

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, atakuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Kwanza la Siku ya Urembo wa Nywele na Ngozi za Asili litakalofanyika Jumamosi wiki hii viwanja vya Makumbusho ya Taifa, Posta, Dar es Salaam.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Eagle Business Consultants ya Dar es Salaam, Antu Mandoza, ilieleza kuwa tamasha hilo lina lengo la kuwahamasisha wanawake wa Kiafrika kuthamini urembo wao wa asili na kuachana na tabia ya kuutukuza utamaduni wa kimapokezi wa kubadilisha mwonekano wao.

Alisema tamasha hilo litakuwa likifanyika kila mwaka na kwamba Julai 28 itakuwa Siku ya Urembo wa Asili kwa kuanzia na Tanzania na baadaye Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

“Onesho hili linalenga kutoa elimu kwa jamii nzima kuhusu madhara ya kiafya ya kutumia kemikali za aina mbalimbali za urembo wa nywele na uchubuaji ngozi, ili kurejesha ujasiri wa zamani wa mwanawake wa Afrika wa kujiamini na kupenda asili yake,” alisema Mandoza.Alisema alianza kampeni ya urembo wa asili kwa kupitia mitandao ya kijamii kuanzia Machi mwaka huu na amekuwa akitumia utambulisho au hashtag yanaturalhairsioushamba.

“Kampeni hii iliungwa mkono na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Ummy Mwalimu.“Mwitikio mzuri wa kampeni ya mtandaoni ndio uliofanya kuzaliwa kwa wazo la kuandaa onesho hili maalumu linalotarajiwa liwe mkombozi wa kizazi kijacho cha Afrika kwa baraka za serikali kupitia kwa Naibu Waziri, Shonza.
“Onesho hili litahudhuriwa na wasanii, wanamitindo na wataalamu mbalimbali akiwemo Dk. Andrew Foi ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi atakayetoa mada kuelezea madhara ya kutumia kemikali katika urembo na kutoa siri za kuboresha nywele na ngozi kwa kutumia vitu vya asili,” alisema.

Kwa mujibu wa muandaaji huyo hakutakuwa na kiingilio chochote na wananchi wote wanakaribishwa na kuongeza kuwa kampuni yake pia inamiliki redio ya mtandaoni iitwayo radio7 www.radio7.co.tz ambayo huelimisha pamoja na kuiburudisha jamii.


Hivyo makala Naibu Waziri kubariki Tamasha la nywele, ngozi za asili

yaani makala yote Naibu Waziri kubariki Tamasha la nywele, ngozi za asili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri kubariki Tamasha la nywele, ngozi za asili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/naibu-waziri-kubariki-tamasha-la-nywele.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Naibu Waziri kubariki Tamasha la nywele, ngozi za asili"

Post a Comment