title : Mratibu wa UN azuru maonesho ya sabasaba
kiungo : Mratibu wa UN azuru maonesho ya sabasaba
Mratibu wa UN azuru maonesho ya sabasaba
MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez ametembelea maonesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam. Akiwa katika maonesho hayo, maarufu kama ya Sabasaba alikutana na Mkurugenzi Mkuu wa Tan Trade, Bw. Edwin Rutageruka.
Katika mazungumzo hayo walijadiliana masuala mbalimbali zikiwamo changamoto na fursa za kibiashara na viwanda zinazojitokeza kwa sababu ya kuwapo kwa maonesho hayo kwa Tanzania na Afrika Mashariki. Baada ya mazungumzo hayo, Mratibu huo alifanya ziara katika mabanda kadhaa akianzia na banda la Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Mwaka huu banda la Umoja wa Mataifa lina wabunifui vijana watatu ikiwa ni sehemu ya shughuli ya Umoja huo ya kuibua na kukuza ubunifu kwa maendeleo endelevu. Ukitembelea banda hilo utakutana na Gracious Fanuel ambaye alivumbua mkono wa roboti ambao unaweza kuendeshwa na simu ya mkononi.
Ni matumaini yake kwamba uvumbuzi huo unaweza kuboreshwa zaidi na kutumika katika viwanda mbalimbali. Mbunifu mwingine ni Latifa Mohammad Ngea kutoka Zanzibar ambaye amevumbua mfumo wa umwagiliaji ambao ni automatiki na inatumia ‘sensa’ kutambua kama ardhi ina unyevunyevu na kupeleka maji katika maeneo makavu.
Pia katika banda hilo la Umoja wa Mataifa utakutana na Amos Mtambala ambaye anatumia uwezo wake wa kiusanii kufanya ujasiriamali. Amos ambaye amefunzwa na kupewa ufadhili na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ametanua shughuli zake na kuingiza vijana zaidi ya 100.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka alipotembelea viwanja vya Sabasaba vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam .
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka katika chumba maalum cha wageni mashuhuri alipotembelea maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (wa pili kulia) pamoja na Afisa Uhusiano wa Shirika la Kazi nchini (ILO), Magnus Minja wakati wakielekea kwenye banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Kazi nchini (ILO), Magnus Minja (kushoto aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez kuhusu uvumbuzi uliofanywa na kijana Gracious Fanuel wa roboti anayeweza kufanyakazi kwa kupitia mifumo ya simu, roboti huyo anaweza kutumika katika shughuli mbalimbali za viwandani wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akiwasilikiliza vijana wabunifu Gracious Fanuel na Latifa Mohammad Ngea kutoka Zanzibar wakati alipotembelea Banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Ofisa wa Mawasiliano kwa Umma wa TanTrade, Daniel Diha wakati alipotembelea Banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akipata maelezo kutoka mwanamke mjasiariamali kutoka Zanzibar alipotembelea banda la SIDO katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Mratibu wa UN azuru maonesho ya sabasaba
yaani makala yote Mratibu wa UN azuru maonesho ya sabasaba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mratibu wa UN azuru maonesho ya sabasaba mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mratibu-wa-un-azuru-maonesho-ya-sabasaba.html
0 Response to "Mratibu wa UN azuru maonesho ya sabasaba"
Post a Comment