title : MHASIBU MKUU WA BODI YA PAMBA NCHINI APANDISHWA KIZIMBANI
kiungo : MHASIBU MKUU WA BODI YA PAMBA NCHINI APANDISHWA KIZIMBANI
MHASIBU MKUU WA BODI YA PAMBA NCHINI APANDISHWA KIZIMBANI
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Mhasibu Mkuu wa bodi ya Pamba Tanzania, Simon Maganga amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka sita likiwemo la uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 55.6 milioni.
Katika mashtaka hayo, mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajili, shtaka moja la ufujaji, ubadhilifu, uhujumu uchumi kusababisha hasara.
Akisoma hati ya mashtaka wakili kutoka Takukuru, Maxi Ali amedai katika shtaka la kwanza kuwa kati ya Januari Mosi, 2009 na Desemba 31, 2010 katika ofisi ya bodi ya Pamba Tanzania iliyopo Wilaya ya Ilala mshtakiwa akiwa kama Mhasibu Mkuu, kwa lengo la kumdanganya mwajiri wake alitumia vocha za kuwasilisha mbegu za Pamba msimu wa 2009/2010 akijaribu kuonesha kampuni ya Afrisian Ginning Ltd ilinunua mbegu za Pamba kilo 25,129,258k wakati akijua kuwa si kweli.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. Imedaiwa,
mshtakiwa huyo akiwa na lengo la kumdanganya mawajili wake alitumia vocha za kuwasilisha mbegu za Pamba msimu wa mwaka 2009/2010 akijaribu kuonesha kampuni ya Nyanza Cooperative Ltd ilinunua kilo 3,708,998 za mbegu za Pamba wakati akijua si kweli.
Pia mshtakiwa Maganga anadaiwa kutumia vocha za kuwasilisha mbegu za Pamba msimu wa mwaka 2009/2010 akijaribu kuonesha kampuni ya kampuni ya S&C Ginning Ltd ilinunua kilo 17,152,590 za mbegu za Pamba wakati akijua si kweli.
Katika shtaka la nne, mshtakiwa huyo anadaiwa kutumia vocha za kuwasilisha mbegu za Pamba msimu wa mwaka 2009/2010 akijaribu kuonesha kampuni ya kampuni ya Kahama Oil Mill Ltd ilinunua 16,326,038 za mbegu za Pamba wakati akijua si kweli.
Katika shtaka la tano inedaiwa, mshtakiwa Maganga akiwa katika ofisi ya bodi ya Pamba Tanzania, alifanya ufujaji na ubadhilifu wa milioni 55,637,680 Mali ya aliyokuwa ameaminiwa na bodi ya Pamba Tanzania.

Mshtakiwa Maganga anadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2009 na Desemba 31,2010 kwa makusudi aliisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh 55,637,680.
Hata mshtakiwa huyo amekana kujibu mashtaka hayo baada ya kuruhusiwa kujibu mashtaka hayo kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka DPP aliwasilisha kibali cha kuipa ridhaa mahakama hiyo kuisikiliza kesi hiyo,
Kufuatia kibali hicho, mahakama imemsomea mshtakiwa masharti ya dhamana ambapo imemtaka
Kuwa na wadhamini wakili kila mmoja akitakiwa kuwa na barua na nakala ya vitambulisho ambapo kila mmoja atatakiwa kusaini bindi ya Sh, milioni 28.
Aidha mdhamini mmojawapo ametakiwa kuwasilisha fedha Sh. Milioni 28 ama hati ya Mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha pamoja na hati yake ya kusafilia.
Kesi imeahirishwa hadi Julai 24,2018.
Hivyo makala MHASIBU MKUU WA BODI YA PAMBA NCHINI APANDISHWA KIZIMBANI
yaani makala yote MHASIBU MKUU WA BODI YA PAMBA NCHINI APANDISHWA KIZIMBANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MHASIBU MKUU WA BODI YA PAMBA NCHINI APANDISHWA KIZIMBANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mhasibu-mkuu-wa-bodi-ya-pamba-nchini.html
0 Response to "MHASIBU MKUU WA BODI YA PAMBA NCHINI APANDISHWA KIZIMBANI"
Post a Comment