MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO

MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO
kiungo : MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO

soma pia


MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara ya siku tano Mkoani Songwe mapema leo na kusisitiza ushirikiano baina ya uongozi ili kuharakisha maendeleo.

Mhe Samia Suluhu Hassan amesema akiwa ziarani katika wilaya za Momba, Mbozi na Ileje amebaini kuwa Mkoa wa Songwe umebarikiwa kuwa na rasilimali na utajiri mkubwa kinachotakiwa ni viongozi kushirikiana katika kuwatumikia wananchi.“Nimefurahishwa na kaulimbiu yenu ya maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kwa ushindani na ushirikiano, bila ushirikiano hakuna maendeleo, kauli mbiu hii sasa ionekane kwa vitendo”, amesisitiza.

Ameongeza kwa kuwataka watendaji na viongozi wote wapende kuwatembelea wananchi kuanzia ngazi za vijiji ili waweze kuwahudumia vizuri na sio kukaa ofisini.Mhe Samia Suluhu Hassan ameongeza kwa kuzitaka halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuwakopesha wanawake na vijana na kubuni miradi mikubwa itayaowaunganisha wajasiriamali wanawake na vijana kutengeneza viwanda ili kuondokana na umasikini.

Amesema mpango wa mkoa wa kuanzisha vituo vya maendeleo vya kata utawezekana na kuwanufaisha wananchi endapo watendapo watajitoa kwa dhati kuufanikisha na mpango huu utaiwezesha Songwe kupaa kiuchumi.

Aidha Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Mkoa wa Songwe kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti na wale walioko mipakani kuendelea kutunza amani.Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa ameshukuru Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kufanya ziara mkoani Songwe kuahidi kuwa maelekezo na maagizo aliyoyatoa atayasimamia yatekelezwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan mapema leo akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Songwe (walioko mstari wa nyuma) kabla hajaondoka kuelekea Mkoa wa Mbeya.


Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO

yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/makamu-wa-rais-ahitimisha-ziara-mkoani_25.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO"

Post a Comment