title : KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAIPONGEZA TTCL KWA KUJENGA MAZINGIRA RAFIKI KWENYE MINARA YA SIMU NCHINI
kiungo : KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAIPONGEZA TTCL KWA KUJENGA MAZINGIRA RAFIKI KWENYE MINARA YA SIMU NCHINI
KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAIPONGEZA TTCL KWA KUJENGA MAZINGIRA RAFIKI KWENYE MINARA YA SIMU NCHINI
Kamati ya Bunge ya Miundombinu imelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujenga mazingira rafiki ya uwepo wa choo na kibanda cha mlinzi kwenye minara ya simu iliyojengwa na Shirika hilo maeneo mbali mbali nchini kote
Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mbatamila kilichopo kwenye kata ya Nampungu wilayani Tunduru mkoani Ruvuma
Mhe. Mchafu amesema kuwa tumeshuhudia kuwa Shirika letu la kizalendo la TTCL pekee ndilo ambalo limejenga miundombinu rafiki ya choo na kibanda kwenye minara yao yote waliyojenga kwenye maeneo mbali mbali nchi nzima kwa ajili ya mlinzi anayelinda minara ya mawasiliano tofauti na kampuni nyingine za mawasiliano ambapo zote kwa pamoja zimepatiwa ruzuku na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ya kujenga minara hiyo kwenye maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara
“Hongereni mmepata mawasiliano ya mnara wa TTCL ambapo wamejenga miundombinu rafiki ya choo na kibanda cha mlinzi cha kupumzikia hivyo mnara utalindwa muda wote, kutakuwa hamna maambukizi ya magonjwa kwa kukosa choo”, amesema Mhe. Mchafu. Ameipongeza TTCL kwa kuwa wamejenga mnara ambao unatoa mawasiliano muda wote kwa kuwa kuna nishati ya jenereta kubwa ya kisasa.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) wakiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme (aliyekaa mbele) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu akisikiliza kwa makini maelezo kutoka Mhandisi wa TTCL mkoa wa Ruvuma Abrahamu Msangi kuhusu mtambo wa mawasiliano ya mnara huo wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati hiyo (hawapo pichani) ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mbatamila kilichopo wilayani Tunduru kwenye mkoani huo
Mkuu wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Albert Richard (wa pili kushoto) akitoa maelezo kuhusu miundombinu rafiki ya mnara wa TTCL kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu (wa tatu kushoto) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mbatamila kilichopo Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu (wa kwanza kushoto) akiongea na wananchi (hawapo pichani) wa kijiji cha Mbatamila kilichopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya mawasiliano wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano mkoani humo. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhandisi Ramo Makani na Mbunge wa jimbo la Tunduru Kaskazini akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mbatimila (wanaomsikiliza) kilichopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo (hawapo pichani) ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo .
Hivyo makala KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAIPONGEZA TTCL KWA KUJENGA MAZINGIRA RAFIKI KWENYE MINARA YA SIMU NCHINI
yaani makala yote KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAIPONGEZA TTCL KWA KUJENGA MAZINGIRA RAFIKI KWENYE MINARA YA SIMU NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAIPONGEZA TTCL KWA KUJENGA MAZINGIRA RAFIKI KWENYE MINARA YA SIMU NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/kamati-ya-bunge-ya-miundombinu_25.html
0 Response to "KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAIPONGEZA TTCL KWA KUJENGA MAZINGIRA RAFIKI KWENYE MINARA YA SIMU NCHINI"
Post a Comment