title : MAHAKAMA KUU KITENGO CHA MAWAKILI WANASTAHILI PONGEZI.
kiungo : MAHAKAMA KUU KITENGO CHA MAWAKILI WANASTAHILI PONGEZI.
MAHAKAMA KUU KITENGO CHA MAWAKILI WANASTAHILI PONGEZI.
Na Bashir Yakub.
Kawaida safu hii huandika na kufafanua masuala mbalimbali ya kisheria na mahakama. Mara nyingi huandika kuhusu ndoa, mirathi, makampuni, jinai, ardhi, na madai mengine kwa ujumla. Leo itakuwa tofauti kidogo japo ni ndani ya tasnia ya sheria humohumo.
Nianze tu kwa kusema kuwa wakati taifa zima likifanya kazi kufikia uchumi wa kati ambao ndio dira ya mihimili yote mahakama,bunge na serikali, kuna jambo moja ambalo hatuwezi kulisahau.
Jambo hili ni utumishi uliotukuka. Hakuna ubishi, injini ya uchumi wa kati ni watumishi. Lakini ni aina gani ya watumishi ambao ni injini ndilo litakuwa swali. Aina ya watumishi ambao wanaweza kutufikisha huko ni wale wenye moyo wa kazi, ari, uvumilivu, waelewa,na wale ambao utumishi kwao sio kazi tu ya kusubiri mshahara mwisho wa mwezi, bali pia huduma nzuri kwa watu.
Kote duniani ambako si tu wamefikia uchumi wa kati tunaoulilia, bali pia wana uchumi wa juu kama china, amerika, na nchi za ulaya wamefikishwa hapo na watumishi bora . Waliowahi kufika huko wanajua ni namna gani watumishi wa huko wanavyotoa huduma. Unaweza kudhani unahudunmiwa na ndugu yako wa tumbo moja.
Niseme tu kuwa watumishi wa mahakama kuu ya Dar es salaam kitengo cha mawakili wameonesha mfano wa aina hii. Ni aina ya watumishi ambao ukibahatika kuhudumiwa nao unahisi kweli umepewa huduma. Hawatachoka kukupatia maelezo, hawatachoka kukuelekeza, na hata ukitaka namba zao binafsi hukupatia, na endapo utapiga muda wowote kutaka ufafanuzi utapewa bila kukaripiwa kama ambavyo imekuwa pahala pengine pa utumishi.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
Hivyo makala MAHAKAMA KUU KITENGO CHA MAWAKILI WANASTAHILI PONGEZI.
yaani makala yote MAHAKAMA KUU KITENGO CHA MAWAKILI WANASTAHILI PONGEZI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA KUU KITENGO CHA MAWAKILI WANASTAHILI PONGEZI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mahakama-kuu-kitengo-cha-mawakili.html
0 Response to "MAHAKAMA KUU KITENGO CHA MAWAKILI WANASTAHILI PONGEZI."
Post a Comment