title : “LAMBALAMBA MARUFUKU MKOANI SONGWE”-CHIKU GALLAWA
kiungo : “LAMBALAMBA MARUFUKU MKOANI SONGWE”-CHIKU GALLAWA
“LAMBALAMBA MARUFUKU MKOANI SONGWE”-CHIKU GALLAWA
Waganga wote wa jadi wanaopiga ramli chonganishi maarufu kama Lambalamba wamepigwa marufuku kufanya shughuli hizo mkoani Songwe huku wenyeviti wa vijiji ambavyo lambalamba watabainika kuendelea na shughuli hizo, hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.
Marufuku hiyo imetolewa mapema leo na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa katika kikao cha wadau wa Afya mkoani hapa ambapo ameeleza kuwa changamoto mojawapo ya sekta ya afya ni uwepo wa waganga wa jadi ambao huwapotosha wananchi kwa imani zisizo za kweli.
Gallawa amesema, “Hatutaki kuona wala kusikia hivi vikundi vya vya lambalamba, kazi yao kubwa ni ulaghai na kuwaibia fedha wananchi, na ninaagiza, mwenyekiti yeyote wa kijiji atakayebainika kuwaendekeza hawa watu tunaanza naye kumchukulia hatua kali za kisheria”.
Ameongeza kwa kuwaagiza wakuu wa wilaya zote mkoani hapa wasimamie kuhakikisha wananchi hawatapeliwi na lambalamba hususani wilaya za Mbozi na Ileje ambako lambalamba wameonekana mara kwa mara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Waganga wa Jadi na Machifu Mkoa wa Songwe Mwenenzunda Mteleshwa amesema kuwa yeye hawatambui lambalamba hivyo serikali iwachukulie hatua za kisheria kwakuwa wanaenda kinyume na taratibu za utoaji wa huduma za jadi.
Mkuu wa Mkoa wa Chiku Gallawa akizungumza katika kikao cha wadua wa Afya kilichofanyika katika chuo cha Uuguzi Mwambani Mkwajuni-Songwe, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremia na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude.
Hivyo makala “LAMBALAMBA MARUFUKU MKOANI SONGWE”-CHIKU GALLAWA
yaani makala yote “LAMBALAMBA MARUFUKU MKOANI SONGWE”-CHIKU GALLAWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala “LAMBALAMBA MARUFUKU MKOANI SONGWE”-CHIKU GALLAWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/lambalamba-marufuku-mkoani-songwe-chiku.html
0 Response to "“LAMBALAMBA MARUFUKU MKOANI SONGWE”-CHIKU GALLAWA"
Post a Comment