title : Kampeni Valisha Mtoto Viatu
kiungo : Kampeni Valisha Mtoto Viatu
Kampeni Valisha Mtoto Viatu
Tarehe 11 April 2018, Best of Zanzibar ilifanya uzinduzi wa Kampeni yake ya Valisha Mtoto Viatu ambayo ilizinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Vuai Ali Vuai, lengo kuu ni kuanza kuwavisha viatu wanafunzi wa skuli za Kijini na Mbuyu Tende ambao zaidi ya 60% wanaenda skuli bila viatu.
Skuli hizo mbili zina jumla ya wanafunzi 1,500 na baada ya uzinduzi wa Kampeni hiyo, wadau mbalimbali walijitokeza kuchangia kampeni hiyo ambapo hadi sasa karibia viatu 900 vimeshachangiwa, Best of Zanzibar inatoa shukrani za dhati kwa wadau mbali mbali ambao wamei-support kampeni hiyo ambayo kwa Kingereza inajulikana kama "A Pair for Every Child Campaign" na hashtag yake ni #PECcampaign
Awamu ya pili ya Valisha Mtoto Viatu imefanyika tarehe 26 -27 Juni 2018 katika Skuli ya Kijini Matemwe ambapo viatu zaidi ya 700 vimeanza kuvishwa kwa wanafunzi wa msingi na baadae Sekondari, Best of Zanzibar kwa kushirikiana na Walimu wa Kijini wamewavisha viatu wanafunzi hao pamoja na kuwaomba kuanzia sasa waweze kuvaa viatu hivyo wanapokuja shuleni.
Best of Zanzibar bado inaungana na kuwakaribisha wadau wote wa maendeleo na jamii kuungana nao katika kuwekeza katika elimu na kuwaomba pia kuwa Mabalozi wao wa Kampeni hii muhimu ya "Valisha Mtoto Viatu" Kwamba, kwa umuhimu wa kampeni hii na kwa kushirikiana na wadau mbali mbali, Best of Zanzibar inaazimia kuifanya kampeni hii Zanzibar nzima kwa skuli za Vijijini kwani ndio wanafunzi wengi wanaenda bile viatu.
Tunashukuru kwa wote waliotuunga mkono na tumeanza kupata Mabalozi kutoka ndani na nje ya Zanzibar kwa Kampeni hii.
Hivyo makala Kampeni Valisha Mtoto Viatu
yaani makala yote Kampeni Valisha Mtoto Viatu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kampeni Valisha Mtoto Viatu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/kampeni-valisha-mtoto-viatu.html
0 Response to "Kampeni Valisha Mtoto Viatu"
Post a Comment