Ileje yapiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni

Ileje yapiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Ileje yapiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Ileje yapiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni
kiungo : Ileje yapiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni

soma pia


Ileje yapiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni

Na Daniel Mwambene, Afisa Habari Ileje
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Joseph Mkude amepiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni,wachungaji na machifu waunga mkono waomba sheria ya kufungua vilabu vya pombe izingatiwe ma wameongezea kuwa wanaovaa “kata K” pia washughulikiwe.
DC Mkude alitoa agizo hilo wakati wa kikao na Muungano wa Jamii Tanzania (MUJATA) kilichofanyika katika Kijiji cha Isoko Kata ya Kafule kikijumuisha viongozi wa dini machifu na wazee maarufu toka Tarafa ya Bundali ukiwa ni mwendelezo wa vikao hivyo vinavyolenga kuifanya wilaya ya Ileje kuwa makazi salama kwa wote.
“Kuanzia sasa ni marufuku kwa watoto kuonekana vilabuni,naagiza kwa watendaji wa kata,vijiji,wazazi na wananchi kwa ujumla,hata kwa watoto wanaobebwa kwani mazingira hayo si rafiki”alisisitiza kiongozi huyo.
Alisema kuwa ubongo wa mtoto anayeshinda maeneo ya vilabuni hauwezi kuepukana na tabia za ulevi kwa vile anaona na kushuhudia namna maisha ya kiulevi yanavyoendeshwa hali atakayoendeleza hata shuleni na hivyo kuzalisha raia wasio wema na kuwa mizigo kwa jamii.
Awali,Paroko Laymond Kapala wa Parokia ya Ipoka aliomba wazazi na walezi wasiwaogope watoto kwasababu ya viwango vyao vya elimu ikiwemo ya Chuo Kikuu.
“Ndugu zangu mmomonyoko wa maadili haujawaacha hata wasomi,sote tunaona vijana wetu wa Vyuo Vikuu wanavyoenenda hata kimavazi hakuna tofauti kati ya msomi na asiye msomi.
Alisema kuwa kamwe mtoto hakui kwa mzaziye hivyo ni jukumu la kila mwanajamii kuvaa viatu vya ulezi ili kuepukana na kupoteza maadili yetu mazuri ya Mtanzania.
Naye Mchungaji Peter Mwakamele wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Isoko aliomba serikali itoe tamko juu ya mavazi ya aibu yanayovaliwa na vijana wakiwemo watumishi wa serikali ukiwemo mtindo wa “kata K”ambao huonesha nguo za ndani kwa wanaume.
Kikao hicho kililenga kujadili kasi ya imani ya” rambaramba” ambalo limeanza kutishia hali ya usalama ya wilaya pamoja na hifadhi ya mazingira kwa serilkali na kwa kuwatumia machifu ambao zamani waliweza kufanikiwa sana.
Huo ni mwendelezo wa vikao katika kutoa elimu kwa jamii na kupata maoni namna maovu yanavyoweza kukomeshwa katika jamii ambapo Mkuu wa Wilaya alishafanya mkutano kama huu kwa Tarafa ya Bulambya ambapo viongozi wa MUJATA Wilaya ya Ileje walimweleza jinsi wanavyoshirikiana na machifu wa nchi jirani ya Malawi katika kupiga vita maovu yakiwemo mauaji ya imani za kishirikina  na albino.
 Washiriki wa kikao cha Muungano wa Jamii Tanzania (MUJATA) kilichofanyika katika Kijiji cha Isoko Kata ya Kafule kikijumuisha viongozi wa dini machifu na wazee maarufu toka Tarafa ya Bundali wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe.
 Washiriki wa kikao cha Muungano wa Jamii Tanzania (MUJATA) kilichofanyika katika Kijiji cha Isoko Kata ya Kafule kikijumuisha viongozi wa dini machifu na wazee maarufu toka Tarafa ya Bundali wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe.
Washiriki wa kikao cha Muungano wa Jamii Tanzania (MUJATA) kilichofanyika katika Kijiji cha Isoko Kata ya Kafule kikijumuisha viongozi wa dini machifu na wazee maarufu toka Tarafa ya Bundali wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe.


Hivyo makala Ileje yapiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni

yaani makala yote Ileje yapiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Ileje yapiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/ileje-yapiga-marufuku-watoto-kuonekana.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Ileje yapiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni"

Post a Comment