title : HATIFUNGANI YA SH.BILIONI 120 YA TMRC YAORODHESHWA DSE
kiungo : HATIFUNGANI YA SH.BILIONI 120 YA TMRC YAORODHESHWA DSE
HATIFUNGANI YA SH.BILIONI 120 YA TMRC YAORODHESHWA DSE
*CMSA yahimiza kampuni kuingia katika DSE
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji amesema kuwa katika kuhakikisha mikopo ya nyumba inaanzishwa nchini, Serikali ikishirikiana na Benki ya Dunia ilianzisha mradi wa kuwezesha kuwepo kwa mfumo wa mikopo ya nyumba.
Dk.Kijaji ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kuorodhesha hatifungani yenye thamani ya Sh.bilioni 120 za Kampuni ya Mikopo ya Nyumba (TMRC) katika Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE).
Amefafanua kuhusu mfumo wa mikopo ya nyumba amesema kuwa mradi huo uitwao mikopo ya nyummba ulilega kuanzisha mifumo wa mikopo ya nyumba kutokana na kufilisika kwa Benki ya Nyumba Tanzania mwaka 1995 ambayo ilikuwa inatoa mikopo ya muda mrefu kwa wateja kwa ajili ya ujenzi wa ununuzi wa nyumba za makazi.
“Mradi huu ulikuwa na maeneo makuu matatu ambayo ni uanzishwaji wa mfumo wa mikopo ya nyumba, uanzishwaji wa mfuko wa mikopo midogo midogo ya nyumba na kuendeleza mfumo wa ujenzi wa nyumba wa gharama nafuu kwa lengo la kupunguzia wananchi gharama za ujenzi na kuwa na nyumba za gharama nafuu,”amesema.
Amefafanua ili kutekeleza malengo hayo matatu Serikali ilikopa jumla ya Dola za Marekani milioni 100 mwaka 2010 kutoka benki ya dunia ili kuwezesha mradi wa mikopo ya nyumba kufikia malengo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji (katikati) akibonyeza kengele leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuorodhesha hatifungan za Kampuni ya Mikopo ya Nyumba(TMRC) yenye thamani ya Sh.bilioni 120 kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE).Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya DSE Jonathan Njau na kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Soko la Mitaji na Dhamana Nicodemas Mkama.
.Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji (katikati) akifafanua jambo wakati hafla ya kuorodhesha hatifungan za Kampuni ya Mikopo ya Nyumba(TMRC) yenye thamani ya Sh.bilioni 120 kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE).Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya DSE Jonathan Njau.
Hivyo makala HATIFUNGANI YA SH.BILIONI 120 YA TMRC YAORODHESHWA DSE
yaani makala yote HATIFUNGANI YA SH.BILIONI 120 YA TMRC YAORODHESHWA DSE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HATIFUNGANI YA SH.BILIONI 120 YA TMRC YAORODHESHWA DSE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/hatifungani-ya-shbilioni-120-ya-tmrc.html
0 Response to "HATIFUNGANI YA SH.BILIONI 120 YA TMRC YAORODHESHWA DSE"
Post a Comment