title : HAPA KAZI TU YAMRUDISHA LETICIA CCM
kiungo : HAPA KAZI TU YAMRUDISHA LETICIA CCM
HAPA KAZI TU YAMRUDISHA LETICIA CCM
Na Khadija Seif , Globu ya jamii.
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Leticia Ghati Mosore pamoja na wajumbe wenzie wanne wamerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) kuunga mkono juhudi za serikali za kuleta chachu ya maendeleo.
Leticia amebainisha sababu mbalimbali zilizowafanya kuhama chama cha hicho na kupongeza utawala wa awamu ya tano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kuona mabadiliko makubwa sana ya kimaendeleo na kiutendaji.
Mwenyekiti huyo amesema "utendaji wa serikali ya Sasa unatendeka Kwa uwazi, ukusanyaji wa mapato ni mzuri ,na hadi Sasa hivi imenunua ndege Kwa Kodi za watanzania na imejenga barabara za juu "fly overs" pamoja na kujenga reli ya kisasa ".
Amefafanua zaidi na kusema serikali iliyopo madarakani imeweza kuwajali wananchi wake kwa kupeleka dawa hospitali zote nchini, imesambaza umeme vijijini kwa mradi wa umeme wa Vijijini ( REA) hayo yote yanatokana na ukusanyaji wa mapato kuwa mzuri .
Ameeleza kuwa upande wa vyama vya upinzani hawazioni juhudi hizo na zaidi wamekaa na kuponda jitihada za serikali huku wakipinga bajeti isipitishwe huku maendeleo yakiwa yanaonekana Kwa macho.
Leticia amefafanua kuwa wameamua kuhama chama cha NCCR Mageuzi Kwa ridhaa yao wenyewe na kuhamia CCM ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Magufuli.
Waliohama chama hicho ni pamoja na Katibu wa chama hicho Kata ya Segerea Lilian Kichunga,Katibu wa Chama cha Wanawake Mossy Kichau, Mwenyekiti wa Jimbo la Segerea Yunes Zacharia pamoja na Mjumbe Vidaline Nicholaus.
Hivyo makala HAPA KAZI TU YAMRUDISHA LETICIA CCM
yaani makala yote HAPA KAZI TU YAMRUDISHA LETICIA CCM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HAPA KAZI TU YAMRUDISHA LETICIA CCM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/hapa-kazi-tu-yamrudisha-leticia-ccm.html
0 Response to "HAPA KAZI TU YAMRUDISHA LETICIA CCM"
Post a Comment