title : HABARI PICHA DC MJEMA AKIZINDUA JUKWA LA CHANGAMKAMWANAMKE ILALA.
kiungo : HABARI PICHA DC MJEMA AKIZINDUA JUKWA LA CHANGAMKAMWANAMKE ILALA.
HABARI PICHA DC MJEMA AKIZINDUA JUKWA LA CHANGAMKAMWANAMKE ILALA.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa katika hafla ya sherehe ya Wanawake wa Changamka Mwanamke,pamoja na Wanawake wa JUKWAA wa wilaya ya Ilala ukumbi wa NNSF Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Picha na Heri ShabaniMkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizindua Mradi wa kilimo cha pilipili Dar es salaam Jana, katika hafla iliyoandaliwa na Taasisi ya Changamka Mwanamke, wengine pichani wanachana wa taasisi hiyo (Pcha na Heri Shabani)
Mwamba wa habari
MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amezindua miradi miwili ya Taasisi ya Wanawake wa Changamka Mwanamke Dar es Salaam jana ili iwawezeshe Wanawake kujikwamua kiuchumi.
Uzinduzi wa miradi hiyo ilifanyika Dar es salaam jana, katika ukumbi wa NSSF ambao ulishirikisha Wanawake wa Changamka Mwanamke Wanawake wa JUKWAA Wilaya ya ILALA na Wajasiliamali.
Katika mafunzo hayo alizindua miradi ya kilimo cha pilipili na viti vya kukodi katika shughuli mbalimbali.
Akizungumza katika hafla ya taasisi ya Changamka Mwanamke Sophia Mjema alipongeza Changamka Mwanamke kwa kuwaunganisha Wanawake pamoja ili waweze kufikia malengo yao ya kujikwamua.
"Tumezindua miradi miwili mikubwa katika taasisi yenu ya Changamka Mwanamke fedha mtakazo pata mtumie kuweza kukuza miradi hiyo ifikie Wakati kila mtu amiliki Mradi wake.
Alisema taasisi hiyo ni kubwa ambayo imeweza kuwaunganisha Wanawake pamoja hivyo aliwataka Washirikiane wasimamie miradi yao vizuri wafikie Malengo yao.
Aidha alisema ili ufikie malengo kila mtu anawaza mikakati aliyojiwekea ,ambapo aliwataka Wanawake wapanue wigo kwa kukuza Miradi waweze kufungua taasisi zao Zitakazowapa kipato.
Aliwataka Wanawake wa Changamka Mwanamke na jukwaa kushirikiana na Serikali ambapo katika Hafla hiyo mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema alisema amekubali
Kuwa mlezi wa Changamka Mwanamke, Pia alinunua pilipili kwa mnada wa shilingi 500,000 cash,kuchangia taasisi hiyo mwingine Mjasiriamali kutoka Jimbo la Ukonga Amina Mbwana Ally yeye alitoa eneo la Shamba ekari mbili ili kuwapa Changamka Mwanamke ili waendeleze miradi
Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Changamka Mwanamke MARIA LUCAS alimpongeza mkuu wa wilaya ya Ilala kukubali kuwa mlezi.
Malia alisema Changamka Mwanamke ilianziashwa mwaka 2016 kwa sasa wanachama 174 kutoka sehemu mbali mbali
Maria alisema dhumuni la kuanzisha taasisi hiyo kumkomboa Mwanamke kutoka mtazamo hasi kwenda mtazamo chanya ,upendo mshikamano na kutimiza ndoto.
Alisemam madhumuni ya Changamka Mwanamke Foundation kumwezesha Mwanamke kujikwamua kiuchumi kuchochea Maendeleo hasa ya Wanawake na mabinti.
"Mikakati ya tasisi yetu tuliojiwekea kuboresha zaidi yetu ya usindikaji pilipili kwa kuanzisha kilimo cha pilipili na usindikaji ili waweze kupata soko la nje ya nchi ,kauli mbiu yetu ya taasisi Wanapenda kujikomboa na kuacha kuota tena na kutimiza ndoto zao"alisema Malia Lucas.
Hivyo makala HABARI PICHA DC MJEMA AKIZINDUA JUKWA LA CHANGAMKAMWANAMKE ILALA.
yaani makala yote HABARI PICHA DC MJEMA AKIZINDUA JUKWA LA CHANGAMKAMWANAMKE ILALA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HABARI PICHA DC MJEMA AKIZINDUA JUKWA LA CHANGAMKAMWANAMKE ILALA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/habari-picha-dc-mjema-akizindua-jukwa.html
0 Response to "HABARI PICHA DC MJEMA AKIZINDUA JUKWA LA CHANGAMKAMWANAMKE ILALA."
Post a Comment