DCB YATANGAZA KUPATA FAIDA YA SH. BILIONI MOJA

DCB YATANGAZA KUPATA FAIDA YA SH. BILIONI MOJA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DCB YATANGAZA KUPATA FAIDA YA SH. BILIONI MOJA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DCB YATANGAZA KUPATA FAIDA YA SH. BILIONI MOJA
kiungo : DCB YATANGAZA KUPATA FAIDA YA SH. BILIONI MOJA

soma pia


DCB YATANGAZA KUPATA FAIDA YA SH. BILIONI MOJA

Said Mwishehe,Globu ya jamii
BENKI ya Biashara Dar es Salaam(DCB) imetangaza kupata faida ya Sh.bilioni moja katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2018 ambacho kimeishia Juni.

Akizumgumza leo Dar es Salaam Mkurugenzi wa Fedha wa DCB Zacharia Kapama amesema faida hiyo ni ongezeko la asilimia 106 kutoka faida ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2017.

"Ongezeko hilo la faida pia lilipatikana kutokana na kuimarika kwa mapato yatokanayo na riba pamoja na yale yasiyotokana na riba.

"Na limechagizwa na mkazo wa benki katika amana za gharama nafuu, usimamizi wa mizania wenye ufanisi, ufunguaji wa tawi la Dodoma na vituo vya huduma, ukuaji wa mfumo wa kibenki wa kidijitali na wa mawakala pamoja na ongezeko la wateja na miamala,"amesema.

Kapama amesema pia mafaniko hayo yametokana na ukuaji wa mikopo ambapo benki hiyo imefanikiwa kuongeza kiwango cha mikopo kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mikopo iliyokuwepo katika Desemba mwaka 2017.

Pia amesema ufanisi wa benki hiyo umeongezeka hasa katika usimamizi wa matumizi ya riba na yasiyo ya riba, ufanisi wa mizania na uboreshaji wa huduma za utoaji wa mikopo.

Amefafanua katika utoaji huduma, benki ya biashara ya DCB imefanikiwa kuongeza idadi ya wateja kufikia 191,133 katika nusu ya pili ya mwaka iliyoishia Juni mwaka 2018 kutoka 188,305 Desemba mwaka 2017.

"Ongezeko hili la wateja 2,828, limechangia kuimarisha mapato ya benki kupitia kuongezeka kwa miamala, amana za kudumu na utoaji mikopo.
Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati benki hiyo ikitangaza faida ya Sh.bilioni 1.0 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2018. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Rahma Gemina na kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa ndani Deogratias Thadei.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala DCB YATANGAZA KUPATA FAIDA YA SH. BILIONI MOJA

yaani makala yote DCB YATANGAZA KUPATA FAIDA YA SH. BILIONI MOJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DCB YATANGAZA KUPATA FAIDA YA SH. BILIONI MOJA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/dcb-yatangaza-kupata-faida-ya-sh.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DCB YATANGAZA KUPATA FAIDA YA SH. BILIONI MOJA"

Post a Comment