title : Benki ya Azania kuendelea kusaidia upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha msimu huu wa maonyesho ya Sabasaba
kiungo : Benki ya Azania kuendelea kusaidia upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha msimu huu wa maonyesho ya Sabasaba
Benki ya Azania kuendelea kusaidia upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha msimu huu wa maonyesho ya Sabasaba
Ni benki ya kwanza ya kiasili inyowezesha huduma zote za kifedha sehemu moja kwenye Kliniki ya Biashara iliyopo kwenye maonyesho ya Sabasaba
Benki ya Azania (ABL) ambayo ni benki binafsi ya kiasili hapa nchini, imeelezea nia yake ya kuendelea kusaidia sekta mbali mbali za kiuchumi kwa kutoa huduma mahususi za kifedha hususani katika kipindi hiki cha maonyeshao ya kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Charles Itembe alisema lengo la benki hiyo ni kutoa huduma za kifedha kwa wazalishaji bidhaa, viwanda pamoja wakulima kwa ajili ya kusaidia kukuza biashara zao.
Kliniki hiyo ambayo itatoa huduma zote za ushauri wa masuala ya kibiashara sehemu moja, imeundwa na mamlaka ya Kuendeleza Biashara Tanzania (TANTRADE)
Ikiwa na kauli mbiu “Kusaidia Maendeleo Endelevu na ukuaji wa Biashara”, Kliniki hiyo itakuwa ni ya kwanza na ya aina yake ambayo itatoa ushauri kwa aina mbali mbali za biashara ikiwa ni pamoja na biashara ndogo, za kati na kubwa ambazo zitakuwa zinashirikim katika maonyesho ya Sabasaba
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akimpongeza Mkurugezi mtendaji wa Azania Bank Charles Itembe mara baada ya uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Naibu waziri wa viwanda na biashara Stellah Manyanya wakifungua kitambaa wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyabiasharaa na wagon waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wakati wa wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Azania Bank wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wakati wa wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Benki ya Azania kuendelea kusaidia upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha msimu huu wa maonyesho ya Sabasaba
yaani makala yote Benki ya Azania kuendelea kusaidia upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha msimu huu wa maonyesho ya Sabasaba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya Azania kuendelea kusaidia upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha msimu huu wa maonyesho ya Sabasaba mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/benki-ya-azania-kuendelea-kusaidia.html
0 Response to "Benki ya Azania kuendelea kusaidia upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha msimu huu wa maonyesho ya Sabasaba"
Post a Comment