title : Balozi wa Korea, Dk Mengi wazungumzia uunganishaji magari ya Korea nchini Tanzania
kiungo : Balozi wa Korea, Dk Mengi wazungumzia uunganishaji magari ya Korea nchini Tanzania
Balozi wa Korea, Dk Mengi wazungumzia uunganishaji magari ya Korea nchini Tanzania
BALOZI wa Korea Kusini, Mh. Geum-Young Song amesema kwamba atasaidia haja ya uwekezaji wa uunganishaji magari nchini Tanzania pamoja na kuiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha tehama kwa nchi za Kusini, Kati na Mashariki ya Afrika.
Alisema hayo kwenye mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo Balozi huyo wa Korea Kusini alisema kwamba atahakikisha anafanya kila kinachowezekana kushawishi makampuni ya magari ya Korea kusini kuanza kuunganisha magari hayo nchini Tanzania.
Dk. Mengi katika mazungumzo hayo alisisitiza haja ya kuanza mazungumzo ya kina ya ushirikiano katika kuunganisha magari kabla ya kuingia katika masuala ya simu zenye utendaji wa kisasa (Smart Phones) na tehama kwa ujumla.
Alisema pamoja na kukubaliana na wazo la Dk. Mengi kuhusu haja ya kuwa na kampuni ya kuunganisha magari nchini Tanzania katika kuelekea uchumi wa viwanda taifa kutengeneza magari yake yenyewe, alisema kama taifa wana mpango wa kusaidia Tanzania kuwa taifa la viwanda likiongoza katika tehama.
Alisema kwa kuwa taarifa na mambo mengi ya habari ndio nguvu kwa vijana kuelekea katika ustawi wangelipenda kuwa na eneo ambalo vijana watalitumia katika kupata maarifa na kuyatumia kuboresha hali zao na kukua kiuchumi.
Katika mazungumzo hayo Dk. Mengi alisema kwamba kuwapo na viwanda vya magari nchini Tanzania ni ndoto yake na kwamba alikuwa amepanga kwenda Sri Lanka kushawishi ushirika katika uunganishaji magari kuelekea kuyatengeneza Tanzania.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi akizungumza na Balozi wa Korea Kusini nchini, Geum-Young Song wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Biashara na Uwekezaji wa Korea, Hong Kyun Lee. Balozi wa Korea, Dk Mengi wazungumzia uunganishaji magari ya Korea nchini Tanzania.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Balozi wa Korea, Dk Mengi wazungumzia uunganishaji magari ya Korea nchini Tanzania
yaani makala yote Balozi wa Korea, Dk Mengi wazungumzia uunganishaji magari ya Korea nchini Tanzania Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Balozi wa Korea, Dk Mengi wazungumzia uunganishaji magari ya Korea nchini Tanzania mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/balozi-wa-korea-dk-mengi-wazungumzia.html
0 Response to "Balozi wa Korea, Dk Mengi wazungumzia uunganishaji magari ya Korea nchini Tanzania"
Post a Comment