title : WAZIRI WA AFYA ASEMA HAKUNA EBOLA NCHINI ILA KUNA HATARI YA KUUPATA
kiungo : WAZIRI WA AFYA ASEMA HAKUNA EBOLA NCHINI ILA KUNA HATARI YA KUUPATA
WAZIRI WA AFYA ASEMA HAKUNA EBOLA NCHINI ILA KUNA HATARI YA KUUPATA
*Akiri kuripotiwa homa ya Chikungunya, Dengue katika Jiji la Dar
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema hakuna ugonjwa wa Ebola nchini ila kuna hatari ya kuupata.
Hivyo amewahakikishia Watanzania kutokuwa na hofu ha kueleza Serikali imeshachukua hatua mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuweka mashine za kupima ugonjwa huo katika mipaka yote nchini na kuweka vituo vya matibabu kote kila mkoa.
Waziri Mwalim ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia homa ya Chikungunya na Dengue ambapo amekiri kuwepo kwa wananchi waliougua magonjwa hayo.Kuhusu Ebola amesema hawajapokea wala kupata taarifa za mtu yoyote kuugua ugonjwa huo nchini.
"Hatuna mgonjwa wa Ebola ila tupo katika nchi sita ambazo zipo hatarini kupata ugonjwa huo kutokana na kupakana na nchi ya Congo ambayo iripotiwa watu 43 kuugua Ebola."Pia kuna muingiliano mkubwa wa watu nchini kwetu.Hivyo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) tupo hatarini kuupata,"amefafanua.
Waziri Mwalim amesema Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla tayari wamejipanga kukabiliana na Ebola kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwamo kuunda timu maalum ya kufuatilia.Pia wametenga maeneo ya kutoa huduma za afya kila mkoa iwapo kutabainika kuna mgonjwa wa Ebola amebainika iwe rahisi kupatiwa matibabu.
Hivyo makala WAZIRI WA AFYA ASEMA HAKUNA EBOLA NCHINI ILA KUNA HATARI YA KUUPATA
yaani makala yote WAZIRI WA AFYA ASEMA HAKUNA EBOLA NCHINI ILA KUNA HATARI YA KUUPATA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA AFYA ASEMA HAKUNA EBOLA NCHINI ILA KUNA HATARI YA KUUPATA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/waziri-wa-afya-asema-hakuna-ebola.html
0 Response to "WAZIRI WA AFYA ASEMA HAKUNA EBOLA NCHINI ILA KUNA HATARI YA KUUPATA"
Post a Comment