title : WAZIRI MKUU ATAKA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO WADHIBITIWE
kiungo : WAZIRI MKUU ATAKA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO WADHIBITIWE
WAZIRI MKUU ATAKA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO WADHIBITIWE

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini kuendelea kutoa mafunzo kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na kupambana na majanga ya moto pindi yanapotokea katika maeneo yao.
Pia ameziagiza Halmashauri zote nchini kuwa na magari ya zimamoto pamoja na magari ya kubeba wagonjwa kwenye vituo vyote vya Zimamoto na Uokoaji katika maeneo yao.Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Juni 8, 2018) wakati alipofanya ziara katika Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura ya Maafa pamoja na Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha mkoa wa Ilala.
Amesema ili kudhibiti wananchi wanaopiga simu za kuomba msaada wa kutaka kuokolewa, huku kukiwa hakuna tukio lolote la janga la moto lililotokea kwenye maeneo yao, ni vema watu hao wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye kumweleza baadhi ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo kuwa ni pamoja na wananchi kupiga simu wakidai kuna ajali ya moto imetokea katika maeneo yao na baada watu wa uokoaji kufika wanabaini ni uongo.
Hivyo makala WAZIRI MKUU ATAKA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO WADHIBITIWE
yaani makala yote WAZIRI MKUU ATAKA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO WADHIBITIWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ATAKA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO WADHIBITIWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/waziri-mkuu-ataka-wanaotoa-taarifa-za_9.html
0 Response to "WAZIRI MKUU ATAKA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO WADHIBITIWE"
Post a Comment