title : WATAKIWA KUSALIMISHA SILAHA
kiungo : WATAKIWA KUSALIMISHA SILAHA
WATAKIWA KUSALIMISHA SILAHA
JOSEPH MPANGALA - MTWARA
Kamanda ya Polisi Mkoa wa Mtwara DCP Lucas Mkondy ametoa wiki mbili kwa wananchii wote wanaomiliki Silaha Bila ya kuwa na Kibali kuhakikisha wanasalimisha Silahahizo katika kituo chwa Polisi au Ofisi ya serikali ya Mtaa na Kijiji Kabla ya Kuanza Msako wa Nyumba kwa Nyumba.
Zoezi hilo Linakuja baada ya kuonekana kuwa silaha hizo zinatumika kwa uwindaji haram ambapo wanyama mbalimbali wamekuwa wakiripotiwa kuuwawa kwa kitumia silaha zisizotambulika.
Akiongea na waandishi wa Habari Mkoani Mtwara kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara DCP Lucas Mkondya amewaomba wenyeviti wa kijiji na mtaa kuhakikisha wanatangazia wananchii wanaowaongoza ilikuweza kusalimisha silaha hizo.
”Tunawapa wiki mbili watu wanaomiliki silha kiunyume na taratibu za kisheria waziwasilishe vituo vya poli au ofisi za serikali za mitaa Tunaanza Msako mkali wa nyumba kwa nyumba lakini pia nitoe ombi kwa watendaji wa serikali ya vijiji kuhakikisha kwamba watu wote wanaomiliki silaha kinyume na taratibu wawatangazie wazisalimishe wazisalimishe hizo silaha Tukikama Silaha katika kijiji chochote basi mwenyekiti au mtendaji au mwenyekiti wa taa katika eneo hilo naye tutamuwajibisha”
Wakati huo huo Jeshi la Polisi Linawashikilia watu 11 kwa Tuhuma za wizi wa pikipiki 7 ambao walikamatwa maeneo mbalimbali na nyingine zikitokea Mikoa ya Lindi,Ruvuma pamoja na Mtwara.
“Nitoe wito kwa wananchii wote ambao walioibiwa Pikipiki waje wazitambue hizi pikipiki ili tuweze kukamilisha Taratibu za kiupelelezi na kuwafikisha mahakamani ,Watuhumiwa hawa wote tupo nao Tunaendelea kuwahoji kuhakikisha kwamba tumesambaratisha kabisa mtandao wa wizi wa pikipiki katika Mkoa wa Mtwara”amesema kamanda Mkondya.
kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara DCP Lucas Mkondya akionesha Pikipiki saba zilizokamatwa baada ya Msako wa jeshi la Polisi
Hivyo makala WATAKIWA KUSALIMISHA SILAHA
yaani makala yote WATAKIWA KUSALIMISHA SILAHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATAKIWA KUSALIMISHA SILAHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/watakiwa-kusalimisha-silaha.html
0 Response to "WATAKIWA KUSALIMISHA SILAHA"
Post a Comment