title : NAIBU WAZIRI MABULA ATAKA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI
kiungo : NAIBU WAZIRI MABULA ATAKA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI
NAIBU WAZIRI MABULA ATAKA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI
Na Munir Shemweta, Nachingwea
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula ameziataka Halmashauri nchini kutenga maeneo ya ujenzi wa nyumba za watumishi yenye miundombinu ili shirika la nyumba la taifa (NHC) liweze kujenga nyumba za gharama nafuu.
Mhe Mabula amesema hayo jana wilayani Nachingwea mkoa wa Lindi wakati wa ziara yake mkoani Lindi kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi pamoja na kuhamasisha ulipaji kodi za ardhi kwa wananchi wa mikoa ya lindi na Ruvuma.
Alisema, Shirika la Nyumba la Taifa halitakiwi kuingia gharama ya kutafuta maeneo pamoja na kuweka miundombinu kwani kwa kufanya hivyo kutalilazimu shirika kujenga nyumba na kuziuza kwa gharama kubwa jambo litakalowafanya watumishi na watu wengine wanaozihitaji kushindwa kuzinunua au kupanga.
‘’NHC haitakiwi kuingia ghrama zozote, halmashauri ndiyo inapaswa kutenga maeneo na kuhakikisha huduma zote muhimu kama maji, barabara, umeme vinakuwepo na Shirika kazi yake iwe kujenga nyumba tu’’ alisema Mabula
Alibainisha kuwa, iwapo halmashauri zitatenga maeneo na kupeleka huduma zote muhimu basi shirika la nyumba litaweza kujenga nyumba kwa gharama ndogo na kuziwezesha halmahauri kuwa na nyumba zake ambazo zinaweza kuuzwa au kuwapangishwa na kubaki kama rasilimali ya Halmashauri.
Amelitaka shirika la nyumba la Taifa kuhakikisha linaingia makubaliano ya ujenzi wa nyumba na halmashauri kwanza kabla ya kuanza ujenzi ili kuepuka kujenga nyumba zitakazokosa mnunuzi kama ilivyojitokeza kwa baadhi ya maeneo jambo linalolipa hasara shirika la nyumba.
‘’kuna maeneo halmashauri zimejengewa nyumba na shirika lakini hazijauzwa sasa utawezaje kujenga nyingine wakati ulizojenga awali hazijauzwa? ‘’ alihoji Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akizungumza wakati wa kikao na watumishi wa sekta ya ardhi katika ofisi ya Mkuu wa wilaya Nachingwea mkoa wa Lindi wakati wa ziara yake ya kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi, kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango na kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Nachingwea Bakari Bakari.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akisalimiana na watumishi mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi wakati ziara yake ya kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi, katika mikoa ya Lindi na Ruvuma, Kulia ni mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia majalada katika ofisi ya ardhi halmashauri ya Nachingwea wakati akikagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi katika mikoa ya Lindi, Kulia ni mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango.
Mkuu wa Kitengo cha kodi wizara ya ardhi Denis Masame akifafanua jambo mbele ya Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula wakati naibu waziri alipofanya ziara ya kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi katika halmashauri ya Nachingwea mkoa wa Lindi
Katibu Tawala wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi Husna Sekiboko akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula katika wilaya hiyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NAIBU WAZIRI MABULA ATAKA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI
yaani makala yote NAIBU WAZIRI MABULA ATAKA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI MABULA ATAKA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/naibu-waziri-mabula-ataka-halmashauri.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI MABULA ATAKA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI"
Post a Comment