title : VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WATAKIWA KUFUATA SHERIA , KANUNI
kiungo : VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WATAKIWA KUFUATA SHERIA , KANUNI
VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WATAKIWA KUFUATA SHERIA , KANUNI
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini na wanachama kutekeleza majukumu yao ya kisiasa kwa kufuata na kuzingatia Sheria na kanuni za vyama vya Siasa.
Taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Jaji Mutungi amesema lazima sheria za nchi kwa ujumla zifuatwe na vyama vyote vya siasa.
Amefafanua kumeibuka tabia ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini kutumia vibaya vyombo vya habari, hususani mitandao ya kijamii kufanya vitendo au kutoa kauli ambazo zinavunja sheria za nchi.
Hivyo ametoa mwito kwa wenye tabia hiyo kuacha tabia hiyo mara moja. "Ninasisitiza kuwa viongozi wa Vyama vya Siasa wasitumie vibaya dhana ya demokrasia na uhuru wa habari."Amesema ieleweke kwamba mtu yeyote anapokiuka sheria za nchi, sheria itachukua mkondo wake bila kujali wadhifa wa mhusika katika chama cha siasa.
Amesisitiza rai yake kwa viongozi wote wa vyama vya siasa na wanachama wote wa vyama vya siasa nchini, ni wajibu wa kila mmoja wao kuelewa katika kutekeleza majukumu yao ya kisiasa wanapaswa kuheshimu sheria za nchi wakati wote ili kudumisha na kukuza demokrasia ya vyama vingi nchini.
"Kwa kufanya hivyo pia, Viongozi hawa watalinda na kuimarisha Amani ya nchi yetu,"amesema Jaji Mutungi.
Hivyo makala VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WATAKIWA KUFUATA SHERIA , KANUNI
yaani makala yote VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WATAKIWA KUFUATA SHERIA , KANUNI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WATAKIWA KUFUATA SHERIA , KANUNI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/viongozi-wa-vyama-vya-siasa-nchini.html
0 Response to "VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WATAKIWA KUFUATA SHERIA , KANUNI"
Post a Comment