title : TRC WAPEWA MIEZI MITATU KUWEKA VIZUIZI MAENEO YOTE AMBAYO RELI INAKATIZA BARABARA ILI KUEPUKA AJALI
kiungo : TRC WAPEWA MIEZI MITATU KUWEKA VIZUIZI MAENEO YOTE AMBAYO RELI INAKATIZA BARABARA ILI KUEPUKA AJALI
TRC WAPEWA MIEZI MITATU KUWEKA VIZUIZI MAENEO YOTE AMBAYO RELI INAKATIZA BARABARA ILI KUEPUKA AJALI
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
SHIRIKA la Reli Tanzania(TRC) limepewa muda wa miezi mitatu kuhakikisha maeneo yote ambayo reli inakatiza barabara kuwe na vizuizi badala ya kutegemea alama peke yake.
Uamuzi huo unakuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu kutokea kwa ajali ya basi kugonga treni mkoani Kigoma na kusababisha watu 10 kufariki dunia na wengine 26 kujeruhiwa.
Maagizo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati anazindua bodi mpya ya wakurugenzi ya TRC.
Hivyo wakati anazungumza na wajumbe hao na watumishi wa TRC amesema ipo haja ya kuweka vizuizi kwenye maeneo ambayo reli inakatiza barabara.
Amesema katika suala la usalama wa raia wa nchi hii gharama isiwe kigezo cha kutowekwa vizuizi hivyo huku akitoa maagizo ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa vizuizi viwe vimewekwa.
"Hakikisheni kunakuwa na vuzuizi kwenye maeneo ambayo reli inakatiza barabara, ile ajali ya Kigoma kama kungekuwa na kizuizi huenda isingetokea.
"Kuwa na alama peke yake haitoshi kwani wapo wengine macho yao hayaoni mbali, hivyo kukiwa na kizuizi hakuna anayeweza kupita,"amefafanua Waziri Mbarawa.
Amesema vizuizi hivyo vinaweza kuwa vya nguzo ambapo kutakuwa na mtu maalum atatakiwa kukaa na hata akilipwa Sh.300,000 kwa mwezi si mbaya na wala si gharama mbele ya uhai wa mtanzania, hivyo vizuizi hivyo vianze kuwekwa mara moja.
Hivyo makala TRC WAPEWA MIEZI MITATU KUWEKA VIZUIZI MAENEO YOTE AMBAYO RELI INAKATIZA BARABARA ILI KUEPUKA AJALI
yaani makala yote TRC WAPEWA MIEZI MITATU KUWEKA VIZUIZI MAENEO YOTE AMBAYO RELI INAKATIZA BARABARA ILI KUEPUKA AJALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TRC WAPEWA MIEZI MITATU KUWEKA VIZUIZI MAENEO YOTE AMBAYO RELI INAKATIZA BARABARA ILI KUEPUKA AJALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/trc-wapewa-miezi-mitatu-kuweka-vizuizi.html
0 Response to "TRC WAPEWA MIEZI MITATU KUWEKA VIZUIZI MAENEO YOTE AMBAYO RELI INAKATIZA BARABARA ILI KUEPUKA AJALI"
Post a Comment