title : TAKUKURU MKOA WA PWANI WAKIRI KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA KUPOKEA NA KUTOA RUSHWA
kiungo : TAKUKURU MKOA WA PWANI WAKIRI KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA KUPOKEA NA KUTOA RUSHWA
TAKUKURU MKOA WA PWANI WAKIRI KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA KUPOKEA NA KUTOA RUSHWA
Na Linda Shebby, Pwani
TAASISI YA Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kasi ya kujihusisha na vitendo vya kupokea na kutoa rushwa imeongezeka katika Mkoa wa Pwani.
Imeelezwa kuwa katika kipindi cha cha Julai 2017 hadi Juni 8 mwaka huu huku Mkoa huo umekuwa na kesi zipatazo 34 zinazoendelea katika Mahakama mbalimbali zilizopo mkoani hapa.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Susan Raymond ambapo ameyataja maneneo yenye kesi hizo kuwa ni Mkuranga ,Kisarawe , Bagamoyo , Rufiji , Mafia , Chalinze na Ikwiriri.
Aidha Kamanda Susan amekiri kuwepo kwa changamoto katika uendeshwaji wa kesi kutoka kwa mashahidi ambao mara nyingi wamekuwa wakiharibu ushahidi pindi kesi hizo zinapofikishwa Mahakamani.
"Hivyo kutokana na ukosefu wa uaminifu kesi nyingi zimekuwa zikipoteza ushahidi na kushindikana kuendelea,"amesema.
Akizungumzia kuhusu kadhia hiyo amesema kuwa TAKUKURU hawatokata tamaa katika kupambana na rushwa na kuahidi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutoa ushirikiano kwenye kesi hizo za kuzuia na kupambana na rushwa.
Amesema kati ya kesi 34 zinazoendelea Mahakamani katika kipindi cha Julai mwaka 2017 hadi Juni 8 mwaka huu kesi 10 ambazo sawa na asilimia 29.4 zinahusu kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa kinachohusiana na kosa la kushawishi, kutoa na kypokea rushwa.
Huku kesi 22 ambazo ni sawa na asilimia 70.7 zinahusu vifungu vingine vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa pamoja na sheria nyinginezo.
Aidha Kamanda amesema katika kipindi hicho kesi nane zimekamilika na kutolewa hukumu na kati ya hizo kesi sita watuhumiwa wamekutwa na hatia ambayo ni sawa na asilimia 75 ya kesi zote Ilizosikilizwa nankutolewa hukumu kwa kipindi tajwa.
Kamanda Susan amesema kuwa zipo hatua za kuwachukulia kisheria watu wanaoharibu ushahidi hivyo ametoa onyo na kusema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayehusika ikiwa ni kufikishwa mahakamani mara moja.
Wakili wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Bwana Joseph Sang'wa hapa anafafanua zaidi juu ya kifungu cha sheria ambacho kinaelezea hukumu kwa shahidi anayepotosha ama kuharibu ushahidi wa kesi yeyote hapa aneleza zaidi.
Hivyo makala TAKUKURU MKOA WA PWANI WAKIRI KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA KUPOKEA NA KUTOA RUSHWA
yaani makala yote TAKUKURU MKOA WA PWANI WAKIRI KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA KUPOKEA NA KUTOA RUSHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAKUKURU MKOA WA PWANI WAKIRI KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA KUPOKEA NA KUTOA RUSHWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/takukuru-mkoa-wa-pwani-wakiri.html
0 Response to "TAKUKURU MKOA WA PWANI WAKIRI KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA KUPOKEA NA KUTOA RUSHWA"
Post a Comment