title : MUHIMBILI KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WANANCHI
kiungo : MUHIMBILI KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WANANCHI
MUHIMBILI KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WANANCHI
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imeandaa maonesho rasmi ya wiki ya utumishi kwa umma kwa mwaka 2018 yenye kauli mbiu ya "Mapambano dhidi ya rushwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi bora ili kufikia malengo ya ajenda 2063 ya umoja wa Afrika na malengo ya maendeleo endelevu."
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel Aligaesha amesema kuwa maonesho hayo yatafanyika ndani ya hospitali ya taifa ya Muhimbili kuanzia Juni 18 hadi 20 mwaka huu na yatafunguliwa rasmi Juni 18 na Waziri mwenye dhamana ya Afya na ustawi wa jamii Ummy Mwalimu.
Aligaesha amesema kuwa maonesho hayo yataonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na hospitali hiyo na wananchi watapata fursa ya kukutana na madaktari bingwa na kupata elimu ya afya na matibabu sambamba na kutoa maoni na malalamiko kuhusiana juu ya huduma wanazopata hospitalini hapo.
Aidha imeeleza kuwa wananchi watapata fursa ya kujua hali ya upambanaji wa vitendo au viashiria vya rushwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi hospitalini hapo na kuwaeleza wananchi mipango iliyopo katika kutoa huduma za afya endelevu.
Maonesho hayo huratibiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na hufanyika kila mwaka na ni moja ya matukio katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo wanachama huadhimisha kwa kuonesha kazizifanywazo na Serikali na taasisi zake.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aligaesha Aminiel akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maonesho ya huduma ya afya katika hospitali ya taifa Muhimbili.
Hivyo makala MUHIMBILI KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WANANCHI
yaani makala yote MUHIMBILI KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MUHIMBILI KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WANANCHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/muhimbili-kuadhimisha-wiki-ya-utumishi.html
0 Response to "MUHIMBILI KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WANANCHI"
Post a Comment