title : TaGLA YASHIRIKI SEMINA YA UKUAJI WA MIJI NA MAJIJI KUTOKA KOREA KUSINI
kiungo : TaGLA YASHIRIKI SEMINA YA UKUAJI WA MIJI NA MAJIJI KUTOKA KOREA KUSINI
TaGLA YASHIRIKI SEMINA YA UKUAJI WA MIJI NA MAJIJI KUTOKA KOREA KUSINI
Na Leandra, Gabriel, Blogu ya jamii
Tanzania Global Learning Agency (TaGLA) ambayo inajishugha na mafunzo kwa njia ya mtandao nchini leo wameshiriki semina iliyoshirikisha nchi 15 duniani.
Huku Tanzania ikiwa nchi pekee iliyoshiriki barani Afrika kwa kukutana kupitia mtandao na kujadili masuala mbalimbali ya ukuaji wa miji huku Korea kusini wakiwa wenyeji wa semina hiyo.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa mafunzo ya mtandao Charles Senkondo ameeleza lengo la semina hiyo iliyoendeshwa na Profesa Heungsuk Choi kutoka Chuo kikuu Korea ni kuangalia mipango mizuri ya ardhi ya jiji na majiji kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye na hata kuleta mvuto kwa wawekezaji.
Ameeleza semina hiyo iliyokuwa inaendeshwa kwa njia ya mtandao wamejifunza kutoka Korea kusini katika kukua kwa miji na majiji hasa wakati huu ambapo taifa limejipanga kukua kiuchumi na upangaji wa miji.
Aidha amesema kuwa wataalamu mbalimbali wameshiriki na wanataraji hapo baadaye washiriki wachache wataenda Korea kujifunza kuhusiana na semina hiyo.Pia semina hizo zitaendelea hadi Agosti mwaka huu, hivyo wadau wajitokeze kujifunza na ametoa rai kwa wananchi kuhusu kubadilika na kujifunza kwani kwa sasa dunia imekuwa kama kijiji.Hivyo kupitia TaGLA wananchi wanaweza kujifunza na kuona ushindani wa kiuchumi kidunia.
Kwa upande wa Ignance Mchallo ambaye ni Mshauri wa mazingira kutoka Legendary International Ltd ameeleza na ameshauri katika kugawana madaraka na utekelezaji wa mipango hasa katika serikali za mitaa kwa kufanya kazi zao katika kukuza maeneo wanayosimamia.Ameongeza kuwa maendeleo na mazingira ni vitu vinavyoenda sambamba na lazima mazingira yahifadhiwe na kupangwa vizuri ili kuvutia uwekezaji na kuyatunza kwa matumizi ya kizazi cha baadaye.
Naye Mwanasheria mwandamizi wa NEMC Manchare Heche ameeleza kufurahishwa na semina hiyo na kueleza kuwa kama taifa lazima tujifunze katika kupanga miji na majiji na kuhifadhi mazingira hasa katika kipindi hiki ambacho taifa limedhamiria katika kukuza uchumi na mazingira hasa ardhi lazima yatunze kwa kuvutia wawekezaji na kwa manufaa ya vizazi vya baadaye na wananchi wapende kujifunza kwa njia ya mtandao kupitia TaGLA.

Mwanasheria wa Mwandamizi (NEMC)Manchare Heche akichangia mada katika mkutano wa mtandao ambao ulihusisha nchi 15 leo jijini Dar as Salaam.

Wandau wa mazingira wakisikiliza mada mbalimbali katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao uliOhusisha nchi 15 leo jijini Dar as Salaam.

Mkurungenzi Mtendaji wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao,Charles Senkondo (katikati) akifafanua jambo mara baada ya mkutano wa mtandao ambao ulihusisha nchi 15, leo jijini Dar as Salaam. Kushoto ni Mshauri wa Mazingira kutoka Legendary International,Ignace Mchallo na (kulia) Mwanasheria Mwandamizi (NEMC) Machare Heche.

Mkurungenzi Mtendaji wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao,Charles Senkondo akizungumza na mwatendaji mbalimbali waliohudhuria mkutano wa mtandao ambao ulihusisha nchi 15,Mwenyeji ikiwa ni nchi ya Korea kusini leo jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

Hivyo makala TaGLA YASHIRIKI SEMINA YA UKUAJI WA MIJI NA MAJIJI KUTOKA KOREA KUSINI
yaani makala yote TaGLA YASHIRIKI SEMINA YA UKUAJI WA MIJI NA MAJIJI KUTOKA KOREA KUSINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TaGLA YASHIRIKI SEMINA YA UKUAJI WA MIJI NA MAJIJI KUTOKA KOREA KUSINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/tagla-yashiriki-semina-ya-ukuaji-wa.html
0 Response to "TaGLA YASHIRIKI SEMINA YA UKUAJI WA MIJI NA MAJIJI KUTOKA KOREA KUSINI"
Post a Comment