title : TAASISIS MBALIMBALI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTUNZA MAZINGIRA
kiungo : TAASISIS MBALIMBALI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTUNZA MAZINGIRA
TAASISIS MBALIMBALI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTUNZA MAZINGIRA
MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan akiwa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Januari Makamba wakikagua mabanda leo katika maadhimisho ya mazingira duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kwenye uhitimishwaji wa siku ya mazingira (Picha zote na Noel Rukanuga)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hasan amewataka viongozi na taasisi kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika uharibifu wa mazingira.
Akizungumza leo katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani Makamu wa Rais Samia amesema kuwa ni muhimu wananchi wakachukua hatua katika kuhakikisha wanayatunza mazingira na hivyo serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na waharibifu wa mazingira.
Awali akizungumza Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Januari Makamba amesema watahakikisha wanaendeleza jitihada za kuyahifadhi mazingira kwa kuwapa elimu wananchi watumie nishati mbadala na kuepuka mayumizi ya mkaa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye ndiye mwenyeji wa maadhimisho ya mwaka huu kitaifa Paul Makonda amesema wakazi wa Dar es salaam ni wachafu na wanatia aibu hivyo tar 1 july ataanzisha oparesheni ya usafi jijini hapa.
Alvaro Rodrigues ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa akiwa amehudhuria kwenye maadhimisho hayo amesema watahakikisha wanaendelea kufanya kazi kwa pamoja na wananchi wote katika kuyatunza mazingira.
Hivyo makala TAASISIS MBALIMBALI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTUNZA MAZINGIRA
yaani makala yote TAASISIS MBALIMBALI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTUNZA MAZINGIRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAASISIS MBALIMBALI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTUNZA MAZINGIRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/taasisis-mbalimbali-zatakiwa.html
0 Response to "TAASISIS MBALIMBALI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTUNZA MAZINGIRA"
Post a Comment