title : Serikali Yatumia TEHAMA Kuokoa Mabilioni ya Shilingi
kiungo : Serikali Yatumia TEHAMA Kuokoa Mabilioni ya Shilingi
Serikali Yatumia TEHAMA Kuokoa Mabilioni ya Shilingi
Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya
Serikali inaokoa takribani shilingi bilioni moja kutokana na kutumika kwa mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika kuwachagua na kuwapingia shule wanafunzi wanaojiunga na kidato cha tano katika shule zote hapa nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalum jijini Mbeya, Mkurugenzi wa TEHAMA, Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali amesema kuwa mfumo huo umejengwa kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ukilenga kuondoa changamoto zilizokuwepo awali ikiwemo malalamiko kutoka kwa wanafunzi wakati wa kupangiwa shule kulingana na ufaulu wao.
“Kwa sasa Serikali inatumia watumishi wasiozidi 20 wakati awali walitumika zaidi ya 300 katika kuwapangia wanafunzi shule za kidato cha tano hali ambayo imepelekea kupungua kwa gharama za uendeshaji wa mchakato huo kwa kiasi kikubwa.” Alisisitiza Kitali.
Akifafanua Bw. Kitali amesema kuwa mfumo huo tangu uanze kutumika umeondoa malalamiko ya kuwepo kwa upendeleo wakati wa kuwapangia wanafunzi shule kwa kuwa kinachozingatiwa ni sifa za mwanafunzi husika na mchepuo anaotaka kuchukua anapojiunga kidato cha tano na si vinginevyo.
Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali akisisitiza jambo kwa washirki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 jijini yanayoendelea jijini Mbeya.
Mkuu wa Timu ya mifumo ya TEHAMA kutoka PS3 Bw. Desderi Wengaa akisisitiza jambo kwa Meneja wa Fedha PS3 Perpetua Ngogo wakati wa mafunzo ya mfumo wa Epicor 10.2 leo jijini Mbeya.
Afisa Usimamizi Fedha Kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Mmaka Mwinjaka akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya mfumo wa EPICOR 10.2 leo jijini Mbeya kwa wahasibu na waweka hazina wa mikoa ya Njombe, Songwe, Katavi na Mbeya.
Sehemu ya awamu ya pili ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa EPICOR 10.2 yanayoendelea Jijini Mbeya ikiwa ni siku ya tatu ya mafunzo hayo.n(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Serikali Yatumia TEHAMA Kuokoa Mabilioni ya Shilingi
yaani makala yote Serikali Yatumia TEHAMA Kuokoa Mabilioni ya Shilingi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Yatumia TEHAMA Kuokoa Mabilioni ya Shilingi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/serikali-yatumia-tehama-kuokoa.html
0 Response to "Serikali Yatumia TEHAMA Kuokoa Mabilioni ya Shilingi"
Post a Comment