Mufindi, PELUM kutoa Hatimiliki za kimila 700

Mufindi, PELUM kutoa Hatimiliki za kimila 700 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mufindi, PELUM kutoa Hatimiliki za kimila 700, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mufindi, PELUM kutoa Hatimiliki za kimila 700
kiungo : Mufindi, PELUM kutoa Hatimiliki za kimila 700

soma pia


Mufindi, PELUM kutoa Hatimiliki za kimila 700

Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa kushirikiana na Shirika la PELUM Tanzania imeanza zoezi la kutoa hatimiliki za kimila zipatazo 747 kwa wananchi wa vijiji vitano vikiwemo vya Usokami, Ugesa, Magunguli, Isaula na Makungu.

Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Mufindi, Simon Mbago ameyazungumza hayo hivi karibuni alipokuwa akihojiwa na Mwandishi wa Habari hii ofisini kwake ambapo amesema kuwa hatimiliki hizo zimeanza kutolewa baada ya wananchi wa vijiji hivyo kufanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi kupitia mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Kusimamia Sekta ya Kilimo unaofadhiliwa na watu wa Marekani.

“Tunalishkuru Shirika la PELUM kwa kufanya kazi nasi kwani limetusaidia kutekeleza moja ya majukumu yetu ya upimaji ardhi na utoaji hatimiliki ambapo hatimiliki hizo zinatarajia kunufaisha wanawake 250, wanaume 385, wenza wenye ushiriki wa pamoja 97 pamoja na maeneo ya Taasisi 15”, alisema Mbago.

Mbago ameongeza kuwa ni jukumu la kila Halmashauri kuhakikisha inatenga fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo ili kuvifanyia vijiji vyake mpango wa matumizi ya ardhi hivyo uwepo wa mashirika binafsi likiwemo la PELUM husaidia kwa kiwango kikubwa kuchochea maendeleo katika Halmashauri mbalimbali.

Pia Mbago amefafanua umuhimu wa hatimiliki hizo kuwa zitasaidia wananchi wa Halmashauri hiyo kuzitumia katika kuomba mikopo kwenye Taasisi za fedha kwa kuweka dhamana maeneo yao pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi kwenye vijiji husika hasa kwa wananchi waliopo mipakani mwa wilaya ya Kilolo na Mufindi.
 Asafu Mgelekwa na Mkewe Atuganule Lunyungu wakiwa wameshikilia hati zao za pamoja.
Simon Mbago Afisa Ardhi Mufindi akimsaidia mwananchi kuweka saini kwenye fomu kama uthibitisho ya kuwa amepokea hati.
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ugesa wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na hatimiliki zao za kimila.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Mufindi, PELUM kutoa Hatimiliki za kimila 700

yaani makala yote Mufindi, PELUM kutoa Hatimiliki za kimila 700 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mufindi, PELUM kutoa Hatimiliki za kimila 700 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/mufindi-pelum-kutoa-hatimiliki-za.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mufindi, PELUM kutoa Hatimiliki za kimila 700"

Post a Comment